Mchungaji
Anthony Lusekelo amefunguka kuhusu tuhuma za yeye kunywa pombe, na
kuweka wazi kuwa hanywi pombe bali anakunywa 'wine' isiyo na kilevi,
huku akisita kusema endapo unywaji pombe ni dhambi au siyo dhambi.
Amefunguka
hilo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, na kuweka wazi
kuwa wanaomtuhumu kuwa yeye anakunywa pombe wanapaswa kutoa ushahidi juu
ya tuhuma hizo, na kwamba unywaji pombe unaweza kuwa dhambi ama usiwe
dhambi kulingana na imani na dini ya mtu.
"Hao
wanaotuhumu kuwa nakunywa pombe, waeleze ni pombe gani nakunywa,
nilikuwa nakuywa wapi na aliyeniona ni nani... kuna sehemu nyingine
pombe siyo dhambi, dini nyingine mpaka kanisani kuna bar".
Je, kunywa bia kiasi bila kulewa ni dhambi au siyo dhambi?
Hilo
ni swali lingine alilokutana nalo kuhusu unywaji Pombe, ambapo katika
majibu yake amesema hawezi kusema kama ni dhambi au lah, maana
inategemea na imani ya mtu, huku akiongeza kuwa Bibilia haijazuia
unywaji pombe
"Inategemea
na makanisa, kuna mengine hata kunywa soda ni dhambi. Dhambi ni
makubaliano yenu kwenye dini yenu. Bibilia inasema kula kitu chochote
hata chakula kama ukila kupitiliza ni dhambi, hata unywaji wa pombe
ukinywa ukapitiliza ni dhambi. Biliblia haijaandika moja kwa moja kwamba
msinywe pombe, imesema msilewe kwa kuwa ndani ya ulevi kuna ufisadi,
cha msingi mbadilishe ulevi wenu uwe ni roho mtakatifu"
Ikumbukwe
kuwa sekeseke lililosababisha Mzee wa upako adaiwe kunywa pombe,
lilihusisha kurushiana maneno na jirani zake ambapo baada ya hapo vyombo
vya habari hasa magazeti yaliripoti tukio hilo kwa namna ambayo Mzee wa
Upako hakuipenda, na hata kufikia hatua ya kuwatabiria kifo waandishi
walioandika habari hiyo.
Alipoulizwa
kuhusiana na ahadi yake hiyo ya kuwatabiria vifo, alisema kuwa tayari
amewasamehe ingawa uwezo wa kuwaombea kifo anao.
"Tulisema
hatuwezi kutumia nguvu kubwa sana kuwaombea watu kifo, kwa sababu sisi
ni wanadamu, na wanadamu tuna mapungufu kwahiyo nikaona ni bora
kumuachia Mungu. Uwezo huo wa kuwaombea watu wakafa, mimi ninao, lakini
nikaona inasaidia nini mtu kumuombea mabaya, kwahiyo nikaamua kusamehe"
Baadhi
ya watu walitaka kujua ni kwanini haendi kuombea wagonjwa hospitalini
ili wapone, ambapo alijibu kuwa maombi hufanywa katika mazingira maalum,
na kwamba hospitali kila mgonjwa ana imani yake.
"Maombi
lazima kuandaa mazingira, na sehemu ambayo Mungu amesema tukutane ni
kanisani, ndiyo maana hata wakati wa Yesu wagonjwa ndiyo walimfuata
Yesu, siyo Yesu aliwafuata wagonjwa.. Kinachoponya ni imani ya mtu, pale
hospitali kila mtu ana imani yake, wakati mwingine hata kumuombea mtu
inabidi umuombe kwanza maana wengine hawapendi kuombewa"
0 comments:
Post a Comment