Mshindi
ya tuzo la Nobel raia wa Nigeria Wole Soyinka, ametimiza ahadi ya
kuirarua green card yake kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Mwezi
uliopta mshindi huyo wa tuzo la fasihi alisema kuwa angeirarua green
card, ambayo humpa mtu kibali cha kuishi nchini Marekanai ikiwa Dionald
Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.
Aliliambia shirika la AFP mjini Johannesburg kuwa kutokana na vile Trump ameshinda, basi ametekeleza alichokisema
"Tayari
nishafanya, nimetoka Marekani , nimefanya kile nilisema ningekifanya,
nilitupa green card yangu , nimerudi penye ninastahili kuwa," alisema
Soyinka.
Hata hivyo Soyinka hawashauri watu wengine kufuata mkondo huo.BBC
0 comments:
Post a Comment