Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kushoto)
akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji
wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) kwenye Ofisi
za Tume zilizoko Posta jijini Dar es salaam. Mhe. Jaji Semistocles
Kaijage ameapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam kuiongoza Tume hiyo
kwa kipindi cha miaka 5.
Watumishi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti mpya wa Tume
hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Posta, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe.
Jaji Semistocles Kaijage (kulia) akiwa Ofisini kwake kwa mara ya kwanza
mara baada ya kuapishwa leo. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa
kuongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 20
Desemba, 2016.
Mwenyekiti
mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe.
Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage akitoa ufafanuzi kwa vyombo vya Habari kuhusu majina 11 yaliyoteuliwa kugombea Ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani Zanzibar na majina 72 ya wagombea Udiwani kwenye Kata 20 za Tanzania Bara. Picha/Aron Msigwa -NEC.
0 comments:
Post a Comment