UN ina walinda amani 16,000 Sudani Kusini
Umoja wa
mataifa imekiri kuwa vikosi vyake vya kulinda Amani Sudani Kusini
vimeshindwa kuwalinda raia katika mji mkuu wa Juba wakati wa mapigono
baina ya pande mbili mwezi Julai.
Afisa wa
kulinda amani Aditya Mehta amesema kwamba wakati kukiwa na wasiwasi
kidogo kuwa vikosi vya umoja wa mataifa vimesaidia kuokoa maisha ya
mamia kati ya maelfu ya raia wa Sudan Kusini, imebainika kwamba
ilihitajika kurejesha amani ya jamii zisizo na ulinzi.
Mapema,
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon alimtimua kamanda wa kikosi
cha kulinda amani baada ya utafiti wa ndani kubaini kuwa vikosi vya
kulinda amani vilikataa kujibu mashambulizi wakati wanajeshi wa serikali
walipowashambulia wafanyakazi wa mashirika ya kigeni ya misaada.BBC
0 comments:
Post a Comment