Rais wa
Rwanda Paul Kagame akiwasha moto wa kumbukumbu katika eneo la kumbukumbu
la mauaji ya kimbari mjini Kigali, wakati wa maadhimisho ya miaka 21 ya
mauaji ya kimbari, Aprili 7, 2015.
Tume ya
Kitaifa dhidi ya Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda imetoa orodha ya
maafisa waandamizi 22 wa Ufaransa ambao inawatuhumu kuhusika katika
mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, katika kukabiliana na uamuzi wa majaji
wawili wa Ufaransa wanaoendesha upya uchunguzi katika shambulio dhidi ya
ndege ya Rais wa zamani Juvenal Habyarimana.
"Maafisa
wa ngazi ya juu wa Ufaransa na wanasiasa walitekeleza uhalifu mbaya
nchini Rwanda," Tume ya Kitaifa dhidi ya Mauaji ya Kimbari (CNLG)
imeshtumu katika ripoti iliyowasilishwa Jumanne kwenye ofisi za shirika
la habari la AFP. Ripoti hii inayojulikana kamai "njama ya kesi ya ndege
ya Habyarimana, Ufaransa yahusika katika mauaji hayo. "
Rwanda
inaishtumu kwa miaka ukadhaa Ufaransa kushiriki katika mauaji ya
kimbari, ambapo watu zaidi ya 800,000, wengi wao wakiwa kutoka jamii ya
Watutsi waliuawa. Shambulizi la Aprili 6, 1994 dhidi ya ndege ya rais,
ambapo aliuawa rais wa kutoka jamii ya Wahutu Juvenal Habyarimana na
mwenzake wa Burundi Cyprien Ntaryamira, linachukuliwa kama tukio
lililozua mauaji ya kimbari.
Lakini
uhusiano kati ya nchi hizi mbili uliingia upya matatani tangu mahakama
ya Ufaransa kuanzisha uchunguzikwa kusikia ushuhuda wa mkuu wa zamani wa
majeshi ya Rwanda, Kayumba Nyamwasa, ambaye anamtuhumu Rais wa sasa wa
Rwanda, Paul Kagame, kwamba ndiye mwanzilishi wa shambulizi dhidi ya
rais Juvenal Habyarimana.
Kwa
mujibu Tume ya Kitaifa ya Kupambana dhidi ya Mauaji ya Kimbari (CNLG),
uamuzi wa hivi karibuni wa Uifaransa kuanzisha upya uchunguzi kuhusu
shambulio dhidi ya ndege ya rais Juvenal Habyarimana Aprili 6, 1994
"inalenga kuficha" ukweli kuhusu kuhusika kwa Ufaransa katika mauaji ya
kimbari nchini Rwanda. Tume hii imetoa orodha ya maafisa wandamizi 22 wa
Ufaransa ambao wanatuhumiwa kula njama bali pia kwa kuhusika katika
mauaji hayo. "Maafisa wa Ufaransa walihusika katika mauaji ya kimbari
kama wahalifu na washirika," CNLG imebaini.
Jenerali
Jacques Lanxade, aliyekuwa Mkuu wa majeshi ya Ufaransa, na jenerali
Jean-Claude Lafourcade, ambaye alikua kiongozi wa kikosi kiliyojulikana
kwa jina la Turquoise Juni 22, 1994 nchini Rwanda chini ya mamlaka ya
Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa maafisa hao waandamizi 22 wanaotajwa
kuwa walihusika katika mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka
1994.
0 comments:
Post a Comment