Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la
Polisi, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu ya operesheni
walizozifanya hivi karibuni leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la
Polisi, Simon Sirro akionyesha bunduki ambayo iliangushwa na wtu
wanaodhaniwa kuwa majambazi leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la
Polisi, Simon Sirro akionyesha kwa waandishi habari begi la bangi
ambalo lilikuwa likiinga Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la
Polisi, Simon Sirro akionyesha panga ambazo wamezikamata katika
operesheni leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la
Polisi, Simon Sirro akionyesha gari la Polisi likiwa linabeba mzigo wa
bangi uliokatwa na Polisi katika msako ulifanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu zaidi ya 200
kwa tuhuma mbalimbali likiwemo kwa watu Raia wa China kutapeliwa dola za
kimarekani 800 kwa kutumia jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda.
Akizungumza
na waandishi wa habari , Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro amesema kukamatwa kwa
watu hao imetokana na operesheni zinazoendelea katika jiji la Dar es
Salaam kuhakikisha wananchi na mali zao wanaishi kwa amani.
Amesema
katika waliokamatwa ni pamoja ni panya road saba waliomvamia Nyumbani
kwa Askari wa Jeshi la Wananchi , Ladislaus Kaitaba.
Katika
tukio waliweza kukamata mtandao wa panya road kwa kutumia Ramadhani
Ndabi (35)ambaye alichukua simu ya askari hiyo baada ya kupiga
akapatikana na kuanza kutaja wenzie wanaofanya matukio.
Aidha
amesema kuwa wizi wa magari unaendelea lakini polisi waliweza kukamata
gari lilokuwa likiuzwa kwa kujifanya wateja na ilipogundulika walioiba
wakatoweka.
0 comments:
Post a Comment