Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kulia)
akiongea na Meneja wa TEMESA Lindi Mhandisi Grayson Maleko (kushoto)
alipotembelea kituoni hapo.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (katikati)
akiongea na Mafundi wa TEMESA Lindi walioko kwenye mafunzo ya vitendo,
alipotembelea kituoni hapo.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto w)
akiongea na watumishi wa Karakana ya TEMESA Lindi, alipotembelea
kituoni hapo mapema.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akiangalia
eneo litakalojengwa gati kwa ajili ya Kivuko cha Lindi Kitundamkoani
Lindi. Picha Zote na Theresia Mwami TEMESA Lindi
Na Theresia Mwami TEMESA Lindi
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu
amepongeza utaratibu unaotumika katika kituo cha TEMESA Lindi na
karakana zake kwa kuratibu vizuri kazi za kila siku.
“Nawapongeza
sana kwa utendaji wenu wa kazi kwa kuweka utaratibu wa kufuatilia kila
kazi inayofanywa na wafanyakazi wa kituo” alisema Dkt. Mgwatu.
Dkt
Mgwatu amemuagiza Meneja wa TEMESA Mkoa wa Lindi Mhandisi Greyson
Maleko kuhakikisha kuwa magari yote ya Serikali mkoani Lindi yanafanyiwa
matengenezo katika karakana ya TEMESA iliyopo mkoani humo.
Dkt.
Mgwatu amemtaka Meneja huyo kuhakikisha anakusanya madeni yote wanayodai
kwenye Taasisi, Halmashauri na Idara mbalimbali za Serikali kutokana na
matengenezo ya magari na mitambo, sambamba na kulipa madeni yote
wanayodaiwa na wazabuni kwa kipindi cha Julai-Septemba, 2016.
Kwa
upande wake Meneja wa TEMESA Lindi alisema kuwa changamoto kubwa
inayokabili kituo hicho ni uwepo wa madeni makubwa wanayodai kwenye
Taasisi na Halmashauri mbali mbali za serikali zilizopo Mkoani Lindi
kutokana na matengenezo ya magari na mitambo lakini wanajitaidi
kuendelea kufanya kazi kwa ustadi na kujituma.
Katika hatua nyingine Dkt. Mgwatu alitembelea eneo litakalojengwa gati kwa ajili ya kivuko kutoka Lindi hadi Kitunda.
0 comments:
Post a Comment