Wapiganaji
kutoka kabila lenye nguvu wamekuwa wakimshambulia yoyote ambaye
wanaamini kuwa ana uhusiano na ISShirika la haki za binaadamu, Amnesty
international, linasema kuwa kuna ushahidi mkubwa kwamba wapiganaji wa
kisuni wanasaidia katika kampeni za kuukomboa mji wa Mosul kutoka
mikononi mwa Islamic State.
Wamekuwa wakilipa kisasi dhidi ya wakazi wa mji huo huku watoto wadogo wakishukiwa kuwaunga mkono wapiganaji wa IS.
Ripoti ya
shuhuda mmoja inasema kuwa wapiganaji kutoka kabila lenye nguvu
wamekuwa wakimshambulia yoyote ambaye wanaamini kuwa ana uhusiano na IS
katika vijiji vilivyokombolewa kusini Mashariki mwa Mosul.
Chanzo
kutoka eneo hilo kililiambia shirika la haki za binadam kuwa wameona
watu wakipigwa, wakipigwa shoti za umeme muda mwingine wakiburuzwa kwa
gari mitaani.
Nje
kidogo Mashariki mwa Mosul, wanajeshi wa Iraq wanafanya msako wa nyumba
hadi nyumba kuona kama kuna mpiganaji yeyote wa IS aliyesalia. BBC
0 comments:
Post a Comment