WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar imesema haijaridhishwa na kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kwa
mitihani ya kidato cha pili na cha nne na kuwataka walimu kubuni
mikakati ya kuongeza ufaulu.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mmanga Mjengo Mjawiri
alisema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Jumbi wilaya ya
Kati Unguja baada ya kufanya ziara kuangalia maendeleo ya sekta hiyo
pamoja na matayarisho ya mitihani ya taifa.
Mjawiri alisema kiwango cha ufaulu usioridhisha kimewavunja moyo
wazazi wengi ambapo moja ya kazi kubwa ya Wizara ya Elimu ni kulipatia
ufumbuzi suala hilo kwa haraka.
“Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar imesikitishwa na matokeo mabaya ya mitihani ya wanafunzi wa
kidato cha pili na cha nne na sasa imeanza kufanya utafiti zaidi kujua
chanzo chake na juhudi za kukabiliana nazo,” alisema.
Aliwataka walimu kuhakikisha wanakamilisha mitaala ya masomo yao kwa
ajili ya maandalizi mazuri ya mitihani kwa wanafunzi na katika
maandalizi wanatakiwa kuhakikisha kwamba masomo yaliyomo katika mitaala
yanafundishwa na kukamilika kwa ajili ya matayarisho ya mitihani ya
taifa.
Katika kufanikisha suala hilo, walimu wakuu wametakiwa kufanya
ukaguzi mara kwa mara kwa walimu wote ili kuhakikisha kila mwalimu
anatekeleza majukumu yake kikamilifu kwa wakati.
Mjawiri aliwataka walimu wa Jumbi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili
na nidhamu na kusema serikali ipo katika hatua za kuyapatia ufumbuzi
malalamiko ya walimu yakiwamo malimbikizo ya madai yao ambayo
yatatekelezwa katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Jumbi, Maimuna Ilyasa alisema wamefanikiwa
kudhibiti utoro kwa wanafunzi ambao hujishughulisha na ajira.
Wanafunzi wa kidato cha pili na nne wa shule za sekondari za Unguja
na Pemba wapo katika maandalizi ya mitihani ya taifa ambayo inatazamiwa
kufanyika mwezi ujao.
Takwimu za wizara, zinaonesha kwamba ufaulu wa wanafunzi kwa mitihani
ya kidato cha nne hadi cha sita inayotayarishwa na Baraza la Mitihani
la Taifa (NECTA) umeshuka kwa asilimia 30.
Monday, October 17, 2016
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya kilim...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akiangalia bamia zilizopandwa na Vijana wanaopata mafunzo katika kambi ya Mkongo leo tar...
-
Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungan...
-
Timu ya Sevilla FC leo wamefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Timu ya...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment