WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema
tayari baadhi ya watu waliotorosha makontena bandarini bila kukaguliwa,
wameitikia agizo lake la kuwataka kujisalimisha na kufanyika ukaguzi ili
kujiridhisha bidhaa zilizokuwemo ndani ya makontena hayo.
Mwishoni mwa wiki, Mwijage alitoa siku nne kwa wafanyabiashara ambao
wanadaiwa kutorosha makontena 100 bandarini, wajisalimishe Shirika la
Viwango Tanzania (TBS) ili yakaguliwe. Ili kutekeleza agizo hilo waziri
huyo aliweka dawati la dharura kutoa huduma hiyo katika siku za
mapumziko.
Alisema wafanyabiashara ambao wangekaidi agizo hilo, wangechukuliwa
hatua stahiki, ikiwa ni pamoja na kulipa faini ya asilimia 15. Ukaguzi
huo ulitakiwa kufanywa na TBS kwa kushirikiana na Tume ya Ushindani
(FCC). Lengo la ukaguzi huo ni kubaini bidhaa zilizoingizwa nchini na
ubora wake.
Alisema kuna wafanyabiashara wanaleta makontena yana nguo, ambazo
zina kiwango cha chini na wengine hawalipi kodi, wengine wanaleta
vilainishi vya magari wakati hapa nchini, pia kuna kiwanda cha kuzalisha
vilainishi hivyo, hivyo kuruhusu makontena kupita bila kukaguliwa ni
kuua viwanda vya ndani.
Aidha, alisema anaipenda sana kazi yake ya uwaziri, ndio maana
analazimika kufanya kazi za chini, ambazo zingefanywa na ofisa wa
kawaida wa Shirika la Viwango (TBS).
Akizungumza jana wakati wa kuzindua Sensa ya Uzalishaji Viwandani ya
Mwaka 2013, Mwijage alisema ili asiondolewe kwenye wadhifa huo na
aliyemteua (Rais John Magufuli), ni lazima afanye kazi hata ya kukagua
makontena kwani anafanya hivyo kwa lengo la kulinda viwanda vya ndani.
“Aliyenipa kazi hii tajiri namba moja, ameniagiza nifanye hivyo, ndio
maana naenda hadi mitaani kukagua makontena kazi ambayo ingefanywa na
ofisa wa kawaida wa TBS,” alisema Mwijage na kutamba kwamba kazi yake
hiyo imezaa matunda.
Alisema licha ya kuwepo baadhi ya watu kumkebehi kwenye mitandao ya
kijamii kuhusu hatua yake ya kwenda mitaani kukagua makontena, alisema
hatishiki kwani yeye kazi yake ya kwanza kuifanya ilikuwa ni ya ukaguzi
na hivyo anaifahamu vyema kazi hiyo.
“Nawaambia hivi nitaendelea kwenda kukagua makontena, niacheni
nifanye kazi yangu, acheni kuniandika kwenye mitandao,” alisema Mwijage.
Aliongeza “Nilianza kazi nikiwa navaa khaki wakati nafanya kazi hiyo
ya ukaguzi, licha ya kuwa leo hii mimi ni waziri, ndio maana niliwaambia
wafanyakazi wa TBS wasiwe na haraka ya kupanda vyeo, nani angejua mvaa
kaki angepanda hadi kuwa waziri.”
Alisema kuna bidhaa zinatoka nje zikiwa hafifu na hazina ubora, zinaingizwa nchini na kubandikwa lebo ya bandia.
“Kwa mfano kuna tomato zinatoka nje hazina ubora, lakini wanaweka
lebo ya bandia, sasa tusipokagua kontena hizi zinaonekana ni bidhaa za
maana kuliko tomato za nyanya za Morogoro ambazo zina ubora wa asili.
“Natoa mwito kwa Watanzania kununua bidhaa zinazozalishwa nchini
kwani zina ubora kuliko bidhaa zinazotoka nje. Tunataka waje na ukaguzi
ufanyike kwa usahihi ili kujua ubora wao, na sisi tutaendelea kunadi
tomato yetu ya hapa nchini na matokeo tukutane huko sokoni,” alisema.
Alisisitiza kuwa yeye pamoja na wizara yake wataendelea kufuatilia
kila kontena linaloingizwa nchini ili kujua ubora wa bidhaa pamoja na
ulipaji wa kodi.
Alisema hana nia mbaya na wafanyabiashara ila anachowataka ni kutaka wafanye biashara katika uwanja sawa wa kibiashara.
Pia alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuhakikisha kwamba hawaleti
nchini bidhaa, ambazo zinatengenezwa na viwanda ambavyo vimeajiri watu
wengi nchini.
Alisema kuruhusu kuleta bidhaa hizo nchini ni kuua viwanda vya ndani
na matokeo yake ndio kunazalishwa vijana wahalifu, kama wale wa kundi la
Panya Road.
Monday, October 17, 2016
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya kilim...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akiangalia bamia zilizopandwa na Vijana wanaopata mafunzo katika kambi ya Mkongo leo tar...
-
Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungan...
-
Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda akikagua ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa vinavyojengwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chak...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment