Na.Alex
Mathias,Dar es salaam.Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF
limeridhia kocha mkuu wa timu ya Taifa Chars Boniphace Mkwasa kujiunga
na klabu ya Yanga endapo kama mwenyewe ataamua kufanya hivyo.
Shirikisho
hilo limeyasema hayo kufuatia uvumi uliopo kwamba uongozi wa Yanga uko
mbioni kumrejesha Mkwasa kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo kufuatia
marekebisho yanayoendelea kufanyika kwenye benchi la ufundi la timu
hiyo.
Msemaji
wa TFF,Alfred Lucas amesema kuwa shirikisho hilo halitakuwa na kikwazo
chochote endapo kocha huyo ataamua kufanya hivyo kwani huenda huko
aindako akapewa kiasi kikubwa cha fedha ikawa tofauti na kile
anacholipwa kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment