METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, October 26, 2016

TFF:MKWASA RUKSA KURUDI YANGA

ek5gmtj2
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limeridhia kocha mkuu wa timu ya Taifa Chars Boniphace Mkwasa kujiunga na klabu ya Yanga endapo kama mwenyewe ataamua kufanya hivyo.

Shirikisho hilo limeyasema hayo kufuatia uvumi uliopo kwamba uongozi wa Yanga uko mbioni kumrejesha Mkwasa kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo kufuatia marekebisho yanayoendelea kufanyika kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.

Msemaji wa TFF,Alfred Lucas amesema kuwa shirikisho hilo halitakuwa na kikwazo chochote endapo kocha huyo ataamua kufanya hivyo kwani huenda huko aindako akapewa kiasi kikubwa cha fedha ikawa tofauti na kile anacholipwa kwa sasa.

Aidha Lucas amesema kwamba ingawa taarifa hizo hazijawa rasmi lkn kama zitakuwepo basi ni vyema Mkwasa akafuata taratibu rasmi za kuvunja mkataba kama alivyofanya wakati anajiunga na timu ya Taifa akitokea klabu hiyo hiyo ya Yanga.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com