Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kulia)
akisikiliza taarifa ya kituo cha TEMESA Iringa kutoka kwa Meneja wa
kituo hicho Mhandisi Ian Makule.
Meneja wa
TEMESA Iringa Mhandisi Ian Makule (Kulia) akimuonesha Mtendaji Mkuu wa
TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) stoo ya vifaa kwa ajili ya ukarabati
mdogo wa magari. Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Iringa
Na Theresia Mwami TEMESA Iringa
Wakala wa
Ufundi na Umeme(TEMESA) imeanzisha program ya kubaini vipuri bandia kwa
ajili ya kuboresha huduma za matengenezo ya magari na mashine
mbalimbali.
Agizo
hilo limetolewa na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt.Mussa Mgwatu
alipotembelea karakana ya TEMESA mkoani Iringa kujionea jinsi karakana
hiyo inayotumia kutumia mfumo huo wa kubaini vipuri bandia.
Dkt
Mgwatu ameongeza kuwa mfumo huu umekuja wakati sahihi kwani kwa sasa
kumekuwa na uingizwaji wa vipuri bandia ambao umesababisha hasara kwa
wamiliki wa vifaa vinavyotumia vipuri kutoka nje ya Tanzania.
“Ili
kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia inabidi tuwe na mfumo
ambao utatusaidia kutambua vipuri bandia kwani vinakwamisha sana
utendaji kazi wetu” alisema Dkt Mgwatu.
Akieleza
jinsi mfumo huo unavyofanya kazi, Meneja wa TEMESA Iringa Mhandisi Ian
Makule alisema kuwa kwa kuingiza taarifa za namba ya gari husika kwenye
program ya kompyuta, unaweza kubaini kama kipuri kinachokusudiwa ni
halisi kabla ya kukiagiza.
Mhandisi
Makule aliongeza kuwa kama namba na jina la kipuri zitakuwa sahihi
kwenye kasha lake lakini kipuri chenyewe sio halisi, kitaweza
kutambuliwa kwa kutumia programu ya ‘barcode scanner’.
Dkt.
Mussa Mgwatu ameziagiza karakana zote za TEMESA nchini kuanza kutumia
programu ya kompyuta katika kuagizia vipuri toka kwa wazabuni ili
kuondokana na lawama zinaotokea wakati wa kutengeneza na kukarabati
magari ya Serikali na mitambo mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment