Msajili
wa Hazina Ndugu Lawrence Mafuru (katikati) akimsikiliza mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa UTT –PID, Ndugu Uli Mtebe wakati akielezea shughuli
za Taasisi hiyo.
Msajili
wa Hazina Ndugu Lawrence Mafuru akipokea mfano wa Hundi kutoka kwa
wakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa UTT – Projects Ndugu Uli Mtebe na Afisa
Masoko wa UTT Projects Bi. Kilave Atenaka kiasi cha shilingi milioni
kumi kwa niaba ya Kamati ya Maafa Bukoba chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.
Msajili
wa Hazina Ndugu Lawrence Mafuru akipokea mfano wa Hundi kutoka kwa
mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa UTT – Projects Ndugu Uli Mtebe kiasi
cha shilingi milioni kumi kwa niaba ya Kamati ya Maafa Bukoba chini ya
ofisi ya Waziri Mkuu. Kulia ni Afisa Masoko wa UTT Projects Bi. Kilave
Atenaka.
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyo chini
ya Wizara ya Fedha,(UTT-PID) imetoa kiasi cha Shilingi Milioni Kumi kwa ajili
ya kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba Mkoani Kagera hivi karibuni.
Tukio hilo la kukabidhi fedha hizo zilizowakilishwa kwa njia
ya mfano wa hundi limefanyika leo Oktoba 7.2016, katika ofisi za Msajili wa
Hazina Jijini Dar es Salaam kwa Msajili wa Hazina.
Awali akipokea ujumbe uliomwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa
taasisi hiyo ya UTT-PID, Msajili wa Hazina Ndugu Lawrence Mafuru ameshukuru
UTT-PID kwa wito wao huo wa kuchangia maafa kwa kuwakumbuka wananchi hao ambao
wengi wao wanahitaji msaada mkubwa.
Naye Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkuu wa UTT –PID, Ndugu Uli Mtebe alimweleza Msajili huyo wa Hazina
kuwa, Taasisi yao imekuwa karibu na watu wa Kagera-Bukoba kwani licha ya
kufanya miradi, pia wamekuwa karibu na jamii hiyo kwa kuwachangia mambo ya
kimaendeleo ikiwemo elimu na miundombinu.
0 comments:
Post a Comment