Naibu
katibu mkuu wa UN wa kitengo cha misaada ya kibinadamu ameilaumu Urusi
na Syria kwa kutumia mabomu mjini Aleppo kuwashinikiza watu
kujisalimisha na kuzua majibizano na Balozi wa Urusi katika Umoja wa
Mataifa.
Majibizano
hayo yalizuka baada ya naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa
anayeshughulikia misaada ya kibinadamu Stephen O´brien kulihutubia
baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusu kile alichokitaja kuwa hali
ya kuogofya katika eneo linalodhibitiwa na waasi la Mashariki mwa
Aleppo ambapo watu 400 wameuawa na takriban watu elfu 2 kujeruhiwa
katika muda wa chini ya mwezi mmoja wengi wao wakiwa watoto.
O'Brien
aliilaumu Syria kwa kuuzingira mji huo na wakati huo huo kufanya
kampeini ya mashambulizi ya mabomu pamoja na washirika wake wa Urusi
katika kampeini ya maksudi ya kufanya maisha ya wakazi wa eneo hilo kuwa
magumu zaidi.
Balozi wa
Urusi katika Umoja wa Mataifa ambaye pia ni rais wa sasa wa Baraza la
Usalama la Umoja huo Vitaly Churkin alijibu akisema tuhuma hizo ni za
kushangaza.
Churkin
ameongeza kuwa inashangaza kwamba O’Brien alizungumzia kuhusu mabomu
hayo kama yanayorushwa hivi sasa katika eneo la Mashariki mwa Aleppo
wakati mashambulizi hayo yalisitishwa kwa siku saba sasa na pia kuleta
dhana kwamba silaha za kemikali zimekuwa zikutumiwa katika mji huo .
Alitaka
kutolewe ushahidi na kumkashifu O’Brien kwa kushindwa kutaja kuwa ngome
ya serikali ya eneo la Magharibi mwa Aleppo limekuwa chini ya kundi la
wanamgambo la al- nusra lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa
al-Qaida.
Balozi wa
Marekani katika Umoja wa mataifa Samantha Power aliongezea sauti yake
katika kuishutumu Urusi na kusisitiza kuwa ilihusika katika mashambulizi
hayo kwa kutumia silaha ambazo hazijawahi kutumiwa hata katika uongozi
wa kiimla nchini Syria. .
Stephen
O’Brien alitoa wito kwa pande zote husika zinazotatiza usaidizi kufika
katika eneo la Mashariki mwa Aleppo na mbinu mbali mbali za mateso
kusitisha hatua hizo na kuruhusu maelfu ya watu waliokwama katika maeneo
mengine 17 nchini humo kupata usaidizi. Marekani, Uingereza na Ufaransa
zilimuunga mkono afisa huyo.DW
0 comments:
Post a Comment