Na Alex Mathias,Dar es salaam
Timu ya
Simba ya jijini Dar es salaam tayari imeshatua mkoani Shinyanga kwa
ajili ya mchezo wao dhidi ya Mwadui FC unaotarajiwa kuchezwa mwisho mwa
wiki hii huku Kocha Mkuu Joseph Omog akitamba kuwa wamekuja kuchukua
alama tatu muhimu.
Akizungumza
baada ya kutua Shinyanga Omog,amesema kuwa nia yetu ni kuendelea kupata
matokeo mazuri kwa kila mechi tunayokutana nayo na sio kwamba
tunadharau wapinzani ila msimu huu tumejiandaa kutwaa ubingwa mapema na
hiyo ndio kiu ya wanasimba.
“Tumekuja
kupambana na kuondoka na alama zote kwa sababu tuna mechi mbili dhidi
ya Mwadui FC na Stand United hivyo hatukuja kutalii na tunajua michezo
yote itakuwa migumu kwetu ila wachezaji wangu wapo kwa ajili ya kupata
ushindi”alisema Omog
Kwa sasa
Simba ndio timu pekee ambayo imecheza mechi kumi na moja bila kupoteza
hata mchezo mmoja na kujikusanyia alama 29 na kuwa kinara wa Ligi huku
wachezaji wakiwa na morali na kiu ya kuchukua ubingwa msimu huu na
wanaonekana kuwa na uchu wa mafanikio.
0 comments:
Post a Comment