Rais
Barack Obama wa Marekani ameyaelezea malalamiko yaliyotolewa na mgombea
kupitia chama cha Republican, Donald Trump, kwamba kuna udanganyifu
unafanyika katika uchaguzi wa Rais nchini humo, kuwa ni ya hatari na
kuharibu demokrasia.
Amemlaumu
mgombea huyo wa Republican kutilia shaka uhalali wa uchaguzi huo, bila
ya kuwa na ushahidi kamili wa kuwepo kwa hila kwenye uchaguzi huo
unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.
Wakati wa
mdahalo wao wa tatu na wa mwisho uliofanyika jana katika yake na
mpinzani wake Hillary Clinton, Bwana Trump alikataa moja kwa moja kusema
kwamba atakubali matokeo iwapo atashindwa.
Hata hivyo chama chake cha Republican kimekuwa kikijaribu kusafisha kauli yake hiyo.
Timu ya
Kampeni ya uchaguzi ya Bwana Trump inamlaumu Hillary Clinton mgombea
kupitia chama cha Democrats kwa kupanga jaribio la kutaka kumchafua
mgombea huyo wa Republican baada ya mwanamke wa 10 kujitokeza akiilaumu
tabia yake ya kudhalilisha wanawake kijinsia.
Mwana
mama huyo Karena Virginia anamtuhumu Bwana Trump kwa kile alichosema
alimpapasa kifuani, wakati wa mashindano ya mchezo wa tenisi mwaka 1998.BBC
0 comments:
Post a Comment