Wakati naruka na Bombadier ya Rwandair kutoka Dar ( Pichani) jana asubuhi, niliziangalia bombadier zetu mbili pale uwanjani na kuanza kutafakari ushindani unaokwenda kukutana nazo kwenye anga.
Jamaa zetu wa Rwanda wamejipanga kwa huduma za ndani ya ndege na ardhini kabla ya abiria kuruka. Wanaposema rwandair.com ( Commercial) kweli wako kibiashara. Sisi na hizi dot.co.tz isije ikawa watendaji wakamuangusha rais wetu kwa kuliendesha shirika ' Kiserikali' badala ya kibiashara.
Kuendesha kusiko kibiashara ni pamoja na mifano ya huko nyuma ya ATC kuchelewa kuruka kwa kuwasubiri waheshimiwa waliochelewa na wamewasiliana moja kwa moja na meneja mkuu! Kubadilisha ruti ghafla kwa ' sababu za kisiasa'. Nauli kulipwa kwa ahadi kwa vile abiria ni ' wa kiserikali' na kadhalika na kadhalika. Hayo ni machache tu...
Maggid.
0 comments:
Post a Comment