METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, October 13, 2016

Mshukiwa wa ugaidi Ujerumani ajinyonga

Polizei Sachsen Fahndungsbild Jaber Albakr (Polizei Sachsen)
Maafisa wanataka majibu baada mshukiwa wa ugaidi kujiua gerezani. Jaber Albakr alipatikana akiwa amejinyonga katika chumba cha gereza alilokuwa akizuiliwa katika mji wa Leipzig.

Waziri wa usalama wa ndani Thomas de Maziere amesema kifo cha Albakr huenda kikavuruga juhudi za kuwasaka washirika wake. Wakili wa Al Bakr Alexander Huebner mwanasheria wa mji wa Dresden, ameliambia gazeti la Focus kuwa gereza la Leipzig lilikuwa linafahamu kuwa mteja wake alikuwa katika hatari ya kujiua baada ya kuonyesha dalili hizo.
 
Mkimbizi huyo kutoka Syria alijiua jana usiku,siku mbili baada ya kutiwa mbaroni.Vyombo vya habari hapa ujerumani viliripoti kuwa mtuhumiwa huyo alifanikiwa kujinyonga japo msemaji wa wizara ya sheria katika jimbo la Saxony Joerg Heroid hakuthibitisha taarifa hiyo au kutoa maelezo zaidi.Mamlaka katika jimbo hilo ilikuwa tayari inakosolewa, baada ya mshukiwa huyo raia wa Syria kufanikiwa kuwakwepa polisi siku ya jumamosi walipokuwa wakijitayarisha kuvamia ghorofa alilokuwa akiishi katika mji wa Chemnitz. Ndani ya chumba alichokuwa akiishi polisi walikuta bomu la uzito wa gramu 1.5 na alikuwa akitumia mtandao kupata maelekezo ya kutengengeza bomu hilo.
Deutschland Polizeieinsatz in Chemnitz nach Sprengsatzfund (DW/N. Conrad)
Jemgo alikokamatwa Jaber Albakr

Jaber Albakr hakuonyesha dalili zozote za kuwa hatari
Albakr, ambaye alikuwa amepewa hifadhi baada ya kuingia Ujerumani mwaka uliopita hatimae alitiwa mbaroni jumatatu wiki hii eneo la Leipiz baada ya raia wengine wa Syria wanaoishi eneo hilo kumfunga kwa kamba na kisha kuwaarifu polisi. Mshukiwa huyo alipewa hifadhi baada ya kuwasili nchini Ujerumani mwaka uliopita na alikuwa akifwatiliwa na wapepelezi tangu mwezi uliopita.Hapo jana waziri wa uslama wa ndani De maziere alisema raia huyo wa Syria alikuwa ameshachunguzwa na kuthibitika kwamba hakuonyesha dalili zozote za kugeuka na kuwa hatari. Maofisa Ujerumani waasema inaaminika mshukiwa huyo alikuwa na ushirikiano na kundi linalojiita dola la Kiislamu IS , na walidhani alikuwa anapanga kuushambulia uwanja wa ndege wa Berlin wiki hii.
default
Uwanja wa ndege wa Schönefeld Berlin

Raia watatu wa Syria waliomtia mbaroni Jaber Albakr w amepewa rasmi uhamisho na waziri de Maizere alisema wanahitaji pongezi na kutambuliwa kutokana na ujasiri wao.Polisi bado wanamzuiliwa mtuhumiwa mwingine anayeshukiwa kupanga shambulizi hilo la bomu lilotibuliwa ambae jina lake limetambulishwa tu kama Khalil A kuambatana na sheria za Ujerumani za kutofichua siri ya mtu binafsi. Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 33 raia wa Syria alikuwa akiishi ghorofa la Chemnitz ambako polisi walikuta bomu hilo .DW
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com