Dkt.Kigwangwalla
akizinduz moja ya kitabu cha Mkakati wa kupambana na magonjwa
yasiyoambukizwa ulizinduliwa jana mkoani Dodoma na kugawiwa kwa waganga
wakuu wote nchini,kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Tamisemi
Dkt.Zainabu Chaula,kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Mohamed
Bakari Kambi
Dkt.Kigwangwalla
akionesha moja ya kitabu hicho kilizhozinduliwa leo na kugawiwa kwa
waganga wakuu wote nchini,kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Tamisemi
Dkt.Zainabu Chaula,kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Mohamed
Bakari Kambi
Naibu Waziri wa Afya akimkabidhi mkakati huo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Profesa Maseru.
Naibu Waziri wa Afya akimkabidhi mkakati huo Naibu katibu Mkuu Tamisemi Dkt.Zainabu Chaula
Dkt.Kigwangwalla akimkabidhi mkakati wa Taifa wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Mohamed Bakari Kambi
ibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi
Kigwangwalla akiwahutubia waganga wakuu wa mikoa na wilaya wakati wa
uzinduzi wa mkakati wa Taifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kwenye
mkutano wa mwaka wa wakuu hao unaoendelea mjini Dodoma
HOTUBA YA NAIBU WAZIRI MHE DKT KIGWANGALA
Napenda
kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kukusanyika hapa siku ya leo.
Pia, ninayo furaha kubwa kusimama mbele yenu kama mgeni rasmi katika
kuzindua mkakati huu muhimu wa pili wa kupambana na magonjwa yasiyo ya
kuambukiza. Pamoja na rasilimali chache tulizonazo, Tanzania imepiga
hatua kidogo katika kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Magonjwa
yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana duniani na
haswa nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwemo. Utafiti uliofanyika na
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa
kushirikiana na Shirika la Afya duniani na Taasisi ya NIMR, ya viashiria
vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza imeonyesha kuongezeka kwa viashiria
hivyo. Idadi ya watu wanaovuta sigara ni asilimia 15.9%, wanaokunywa
pombe ni asilimia 29.3%, wenye uzito uliopita kiasi 34.7%, shinikizo la
damu ni asilimia 25.9% na wagonjwa wa kisukari ni asilimia 9.1%. Hii
haikubaliki, na ni lazima tuongeze bidii katika kuyashughulikia.
Mkakati
huu umekuja wakati muafaka, wakati tunatakiwa kutekeleza Mpango wa
Malengo endelevu (Sustainable Development Goals) ambayo kati ya malengo
kumi na saba, matatu yanazungumzia jinsi ya kupambana na magonjwa yasiyo
ya kuambukiza, baadhi ya malengo haya ni;
Kufikia mwaka 2030, kupunguza moja ya tatu ya vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kukinga, kutibu na kuzingatia afya ya akili;
Kuboresha huduma za kinga na tiba ya utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe;
Kufikia mwaka 2020, kupunguza nusu ya idadi ya vifo duniani na ajali za barabarani.
Napenda
kutambua mchango mkubwa uliotolewa na Chama cha kupambana na ugonjwa wa
kisukari duniani (World Diabetes Foundation) na chama cha kisukari cha
Tanzania (Tanzania Diabetes Association), kwa kuwezesha kupitiwa kwa
mkakati wa zamani wa mwaka 2008-2015, na kutengenezwa huu wa sasa, ambao
ni wa 2016-2020. Kwa kushirikiana na kitengo cha magonjwa yasiyo ya
kuambukiza, TDA imeweza kutekeleza mpango wa magonjwa yasiyo ya
kuambukiza nchi nzima.
Aidha
nawashukuru kwa dhati wadau wetu wa Maendeleo kwa misaada mbalimbali
ambayo imechangia katika kuboresha Afya za Watanzania.
Ninayo
taarifa kuwa Waganga wakuu wa mikoa na wilaya mmeombwa kuteua mtu mmoja
atakayeratibu shughuli zote za magonjwa yasiyo ya kuambukiza mikoani na
wilayani kwenu. Ni matarajio yangu kuwa mtafanya kazi kwa nguvu na kwa
ukaribu zaidi na kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza cha Wizara
ili huduma hizi ziwafikie watu wote hadi ngazi ya jamii.
0 comments:
Post a Comment