Tukio
la msanii wa muziki wa Bongo Fleva, kuzimiwa kipaza sauti wakati aki
perform jukwaani,hapa mjini Mombasa, limeusishwa na imani za
kishirikina.
Akifanya
mahojiano na kituo kimoja cha radio nchini Kenya, Mganga mashuhuri wa
jadi kutoka nchini Tanzania, aitwaemuungu wa kabili, alinukuliwa akisema
kuwa “ Suala la Ali Kiba ni suala la kichawi “, asisingiziwe Sallam
meneja wa Diamond wala Diamond mwenyewe, wala waandaaji wa tamasha, wala
walinzi wa Chris Brown.
Muungu
wa Kabili ambae inadaiwa, alikuwa akiongoza kikosi cha jadi
kinachoundwa na waganga mbalimbali kutoka nchini Tanzania na Kongo ya
mashariki, alikuwepo jijini Mombasa, kuongoza kamati ya ufundi katika
kuhakikisha tamasha hilo linafanyika bila kutokea kwa shari yoyote inayo
weza kusababishwa na wachawi au maadui kama vile kunyesha kwa mvua ya
kichawi, kutokea kwa stampede ( kiwewe kinachopelekea watu kukanyagana
na kufa ), nakadhalika.
Lakini
hata hivyo alipoulizwa kuhusu jambo hilo hakukubali wala kukataa ingawa
anasema alikuwepo jijini Mombasa kwa kikazi na alikuwa mmoja wa watu
walio hudhuria tamasha hilo.
Muungu
wa Kabili aliongeza “ Wachawi na washirikina wanapenda sana kuhudhuria
kwenye matukio yenye kuhusisha idadai kubwa ya watu kama vile matamasha
ya muziki, mikutano ya kisiasa nakadhalika, kwa saabu katika maeneo
hayo, kuna vitu vingi sana vya kichawi na kishirikina ambavyo wachawi
huvichukua kwa ajili ya matumizi ya shughuli zao za kichawi “
“Mfano
wa mambo ambayo wachawi huyafuata kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu ni
pamoja na mchanga, udongo pamoja na mabaki ya vitu vilivyopo katika
eneo la tukio.” Aliongeza muungu wa kabili.
Mchanga
ama udongo wa kwenye eneo lenye mkusanyiko mkubwa wa watu ambao
wamekesha hadi asubuhi huchanganywa na dawa zingine za kichawi kwa ajili
ya kutengeneza ndumba za biashara na kufanyab biashara zitoke sana.
Ilhali
uchafu uchafu na mabaki ya kwenye eneo lenye mkusanyiko mkubwa wa watu,
hutumiwa na watu wa mazingaombwe kwa ajili ya kutengeneza viini macho.
Alieleza muungu wa kabili.
Akizungumzia kuhusu tukio la Ali Kuzimiwa kipaza sauti na kushushwa jukwaani bila ridhaa yake, muungu wa kabili alisema.
“
Uzuri ni kwamba, nilikuwepo katika eneo la tukio na nilishuhudia kila
kitu. Katika mikusanyiko mikubwa ya watu ambayo inakesha huwa kuna
shughuli nyingi sana za kichawi na kishirikina. Kama hauna macho ya
kiroho, hauwezi kuona kinacho endelea.”
Una
jua katika uchawi huwa kuna vitu vinaitwa “ Mamlaka za kichawi”.
Mamlaka za kichawi zinahusisha mambo mengi sana. Miongoni mwa mambo hayo
ni pamoja na mambo ambayo wachawi huyatumia kulogea watu. Unajua mchawi
hawezi kuloga mtu bila kufananisha ulozi wake na kitu kingine.
Kwa
mfano , katika uchawi wa kuwatenganisha watu kama vile wanandoa, ndugu
au marafiki, na kuwa fanya wasionane tena hadi wanarudi kaburini,
wachawi hufanya matambiko maalumu, kasha hutafuta nyayo za watu walio
kusudia, nyayo hizo zinafanyiwa ulozi, halafui unyayo wa mtu mmoja
utakwenda kuzikwa kwenye mlima mmoja, ambao labda upo Mombasa, na unyayo
wa mtu mwingine utaenda kuzikwa kwenye mlima ambao labda upo, NAIROBI.
Sasa
katika ulozi wao, wachawi watasema maneno kama vile “ FULANI BIN
FULANI, SIKU YA LEO NIMEKUZIKA, KATIKA MLIMAA HUU ULIOPO HAPA MOMBASA,
NA FULANI BIN FULANI YEYE AMEZIKWA KWENYE MLIMA FULANI ULIOPO HUKO
NAIROBI. KAMA MLIMA HUU ULIOPO HAPA MOMBASA, UNAWEZA KUKUTANA NA MLIMA
ULIOPO NAIROBI, BASI NA WEWE FULANI BIN FULANI AMBAE NIMEKUZIKA KATIKA
MLIMA HUU, UTAWEZA KUKUTANA NA FULANI BIN FULANI AMBAYE YUPO NAIROBI.
LAKINI
KWA KUWA WEWE FULANI BIN FULANI AMBAE UMEZIKWA KWENYE HUU MLIMA ULIOPO
HAPA MOMBASA, HAUWEZI KAMWE KUKUTANA NA FULANI BIN FULANI, AMBAE
AMEZIKWA HUKO NAIROBI.BASI HATA W EWE FULANI BIN FULANI HAUTAKUTANA NA
FULANI BIN FULANI MPAKA SIKU UNAINGIA KABURINI “
Mifano ipo mingi sana. Haya mambo ya kulinganisha katika ulozi yapo ya aina mbili, Yapo ya asili na yapo ya kutengeneza.
Turudi
kwa Alikiba na kuzimiwa kipaza sauti Mombasa. Kwenye mikusanyiko ya
watu wengi, wachawi hutuma majini kwa ajili ya kuwaangusha au kuwaua
watu, na kisha baada ya hapo, kutumia udongo , au mabaki yaliyopo katika
eneo husika, katika kutengeneza uchawi wa aina mbalimbali kama vile
kifafa cha kichawi, au kushusha nyota.
Uchawi
huu hutumwa katika eneo husika, na hunuizwa watu kuanguka,kuzimia au
hata kufa. Walengwa wakuu wa uchawi huu ni watu maarufu.
Tukio la Ali Kiba, katika ulimwengu wa kiroho lina ashiria, kuzimwa na kushushwa nyota yake kwa nguvu.
Kuzimiwa kipaza sauti kunaashiria kuzimwa kwa nyota yake na kushushwa jukwaani kuna ashiria kushushwa nyota yake.
Tukio hili halikukusudiwa kwa Ali Kiba, ni uchawi ulionuiziwa kwa watu wote katika eneo hilo, sema Ali Kiba amekuwa mhanga tu.
Hii
maana yake ni kwamba, wachawi wataenda kuchukua mchanga katika eneo
hilo, na watautumia kutengeneza uchawi wa kushusha na kuzima nyota za
watu.
Siku
ya tukio, sio Ali Kiba pekee, wapo watu wengi tu walio anguka tena
wenyewe, lakini kwa sababu sio maarufu, Ali Kiba ndio alionekana.
Hii
haimaanishi kuwa Ali Kiba ameshushwa nyota yake la hasha. Nyota yake
itaendelea kuwa juu na ataendelea kufanya vizuri katika shughuli zake za
muziki.
Wachawi
watatumia tukio la kushushwa na kuzimiwa kipaza sauti. Kwa mfano “ Kama
fulani bin Fulani, pamoja na kwamba yupo juu , lakini alizimiwa kipaza
sauti na akashushwa chini, basi hata Fulani bini Fulani nae pia nyota
yake itazimwa na kushushwa.
Alipoulizwa
kuhusu kuwepo kwa taarifa kwamba meneja wa Salam ndio alifanya fitna
ili Ali Kiba azimiwe microphone pamoja na madai kwamba, walinzi wa Chris
Brown ndio walishinikiza Ali Kiba ashushwe,muungu wa akili alisema.
“
uchawi ni unafiki. Hizo sababu unazo zitaja ni unafiki na sio kweli.
Wachawi hutumia busara sana wanapo fanya mambo yao, siku zote huwa
hawataki kujulikana ndio maana huwa wanatengeneza sababu mbadala, ili
watu wasiwastukie.
Mfano wakitaka kukuchukua msukule, watakutengenezea sababu kama vile ajali au ugonjwa wa ghafla nakadhalika.
Mfano
mzuri ni ule wa kwenye maandiko matakatifu, Ndugu zake Yusufu mwana wa
Yakobo, walipo muuza ndugu yao utumwani, walitengeneza uongo wa kupeleka
kwa baba yao kwamba, Yusufu ameuwawa na Simba.
Katika kusapoti uongo wao, wakararua nguo za Yusufu, wakachinja damu ya kondoo na kupaka kwenye nguo za Yusufu.
Baba
ya Yusufu alivyo tazama nguo za mwanae zilizo tapakaa damu, akaamini
kabisa motto wake amekufa, kumbe ameuzwa utumwani. Hiyo ndio hekima ya
kishetani inayo tumiwa na wachawi.
NINI
SULUHISHO KWA ALIKIBA : muungu wa kabili anasema “ Katika ulimwengu wa
kiroho, Ali Kiba haja athiriwa chochote na tukio la Mombasa, lakini ni
muhimu awatafute masheikh, wamfanyie kisomo maalumu na ibada..
Miezi
kadhaa iliyo pita, mwanadada mmoja alitoa ushuhuda wake kupitia vyombo
mbalimbali vya habari, akimlaumu muungu wa kabili kwa kumfanyia madawa
ya kichawi ambayo yalimletea matatizo makubwa katika maisha yake.
Maelezo ya mwanadada huyo yalibeba kichwa “ NILIMLISHA MUME WA MTU LIMBWATA LA NYAMA YA BUNDI “ na yanapatikana mtandaoni.
0 comments:
Post a Comment