Mtendaji
Mkuu wa TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kushoto) akizungumza na Meneja wa
TEMESA Dodoma, Mhandisi Bikulamchi (kulia) alipomtembelea ofisini kwake.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (mbele
aliyekaa) akizungumza na watumishi wa TEMESA Dodoma, katika ukumbi wa
TEMESA Dodoma, alipotembelea kituoni hapo.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu(katikati)
akiangalia kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa karakana mpya ya kisasa
itakayojengwa Mkoani Dodoma kushoto ni Msaidizi wa Meneja Bw. Hassan
Sumbi na Kulia ni Meneja wa TEMESA Dodoma Mhandisi Bikulamchi. Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Dodoma.
Na Theresia Mwami TEMESA Dodoma
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka
watumishi kuanza kujiandaa kwa kupokea kazi nyingi kwani hadi sasa
Serikali na Taasisi zake tayari zimeanza kuhamia Dodoma.
Alisema
kuwa kuhamia Dodoma kutaleta changamoto mbali mbali katika utoaji huduma
za matengenezo ya magari, umeme, elektroniki na viyoyozi kwani mahitaji
ya wateja yatakuwa ni mengi mno kuliko ilivyo sasa.
Dkt.
Mgwatu alizungumza hayo alipotembelea kituo cha TEMESA mkoani Dodoma
kuona changamoto na utendaji kazi na kuzungumza na watumishi wa kituo
hicho.
“Tuanze
kujiandaa kwa ajili ya changamoto hizo, tusingoje kuulizwa kwanini
hatukujiandaa wakati tunafahamu kuwa serikali inahamia Dodoma na naomba
mjipange kutoa huduma ipasavyo” Alisema Dkt. Mgwatu.
Aidha
Dkt. Mgwatu amemuagiza Meneja wa TEMESA Dodoma Mhandisi Bikulamchi
kuanza kuandaa utaratibu wa namna ya kuendeleza kiwanja cha TEMESA
Dodoma kilichopo eneo la Kizota ili kuweza kukabiliana na changamoto ya
mahitaji ya mji wa Dodoma yanayozidi kukua siku hadi siku.
“Ni
mategemeo yangu kuwa katika kiwanja hicho tutaweza kujenga karakana
kubwa tena ya kisasa ambayo itakuwa mfano mkoani hapa, ambayo itaweza
kukidhi mahitaji yote ya soko la mkoa huu na hata nje ya mkoa, sambamba
na ujenzi wa ofisi mpya ya TEMESA Makao Makuu” alisistiza Dkt Mgwatu.
Kwa
mujibu wa Dkt. Mgwatu karakana hiyo ya kisasa ikijengwa itakuwa na
watumishi wa ufundi na utawala kwa uwiano mzuri wenye kuzingatia taaluma
husika ili kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu. Aliongeza kuwa
itatakiwa kufanyika mabadiliko makubwa ili kuweza kuwapata watumishi
watakaoweza kuendana na kasi ya mabadiliko hayo katika kituo hicho.
Pia Dkt.
Mgwatu aliwataka watumishi wa TEMESA Dodoma kufanya kazi kwa kuzingatia
taaluma walizo nazo, kuheshimu taaluma za wengine pamoja na kuzingatia
maadili ya kazi, kufanya kazi zenye ubora ili kuhakikisha wateja
wanaridhika na kazi za TEMESA na hivyo kuvutia wateja zaidi hata kutoka
nje ya Taasisi za Serikali.
Kwa
upande wao wafanyakazi wa TEMESA Dodoma wamemuahidi Dkt. Mgwatu kufanya
kazi kwa bidii zaidi ili kuongeza mapato ya kituo na kwa ubora wa kazi
ingawa bado kuna changamoto ya kupatikana vitendea kazi vya kisasa
katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
0 comments:
Post a Comment