Eneo la kumbukumbu la mashujaa katika mji wa Mekele, Ethiopia
Nchini
Ethiopia, marubani wawili wa ndege za Eritrea walitoroka na ndege zao
Jumatano wiki hii asubuhi na kutua katika uwanja wa Makele, mji mkuu wa
jimbo la Tigre, ambapo waliomba mara moja hifadhi.
Luteni
Mebrahtu Tesfamariam na Luteni Fishaye Afeworki waliondoka Jumatano saa 4
saa za Erutrea katika kambi ya kikosi cha anga mjini Asmara, mji mkuu
wa Erytrea. Walitumia ndege ndogo ya mafunzo aiana ya Zlin 143L,
iliyotengenezwa nchini Jamhuri ya Czech.
Lakini
saa moja baadaye, waliwasilianamamlaka ya uwanja wa ndege wa Mekele,
nchini Ethiopia, katika upande wa pili wa mpaka, na kuomba ruhusa ya
kutua. Ruhusa ambayo walipewa, wakati ambapo, kwa mujibu wa shahidi
mmoja, ndege moja ya kijeshi ya Ethiopia ilipaa angani kwa ajili ya
kukabiliana na uwezekano wa tishio.
Maveterani
Kwa
mujibu wa wenzetu kutoka kituo huru cha Radio Erena, maafisa hao wawili
ni maveterani, ambao wana miaka mingi ya ya kazi hiyo. Afisa wa kwanza
alijiunga na jeshi mwaka 1999 na alifundishwa kuendesha moja ya kivita
aina ya Migs-29 ya Eritrea. Afisa wa pili alijiunga na jeshi la anga
mwaka 2002, chanzo hicho kimesema.
Hii si
mara ya kwanza marubani wa Eritrea kukimbilia nje ya nchi wakiwa na
ndege zao. Marubani kadhaa wa helikopta, na hata rubani wa ndege ya rais
na naibu wake, walikimbilia mafichoni nchini Saudi Arabia katika miaka
ya hivi karibuni.
Itafahamika
kwamba hali ya manung'uniko inaripotiwa katika mamlaka ya usafiri wa
anga nchini Eritrea tangu kufungwa kwa mwanzilishi wake, Meja Habtezion
Hadgu mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia ya kumuomba Rais Isaias
Afewerki kulegeza udikteta nchini humo.RFI
0 comments:
Post a Comment