Katibu
wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa Kamati Maalum ya NEC, CCM
Zanzibar, Hamad Yussuf Masauni akizungumza na viongozi wa Kamati ya
siasa ya Wilaya ya Mjini kichama katika ofisi za Wilaya hiyo Makadara.
Katibu
wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa Kamati Maalum ya NEC, CCM
Zanzibar, Hamad Yussuf Masauni, akikagua ujenzi wa Barabara ya ndani
katika maeneo ya Boznia Kikwajuni Zanzibar.
Katibu
wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa Kamati Maalum ya NEC, CCM
Zanzibar, Hamad Yussuf Masauni, uzinduzi wa mradi wa Maji safi na
salama katika tawi la CCM Sebleni Mwembeboso jimbo la Kwahani Zanzibar.
Na Is-haka Omar, Zanzibar
KATIBU wa
Idara ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa Kamati Maalum ya NEC, CCM
Zanzibar, Hamad Yussuf Masauni amewataka wananchi kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na serikali zote mbili ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Zanzibar ili ziweze kuwaletea maendeleo endelevu.
Kauli
hiyo ameitoa katika mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa Chama
katika Wilaya za Mjini na Amani kichama, alisema endapo wananchi
wataendelea kuziamini na kutoa ushirikiano wa dhati kwa serikali hizo
maendeleo ya nchi yataimarika kwa haraka.
Alieleza
kuwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 unaofanywa na
serikali katika maeneo mbali mbali nchini umetokana na sera pamoja na
miongozo mizuri iliyowekwa na CCM.
Masauni
Ambaye pia ni Mbunge wa tiketi ya CCM jimbo la Kikwajuni alieleza kuwa
CCM ndio chama pekee chenye sera za kuwaunganisha wananchi wa Tanzania
na Zanzibar kwa ujumla ili waishi kama watu wa taifa moja lenye uwezo na
nguvu za kijamii na kiuchumi.
“CCM itaendelea kuwa imara endapo tutakuwa wamoja na wenye nia thabiti ya kulinda amani na utulivu wa nchi zetu.
Pia sote
ni mashahidi juu ya juhudi zinazofanywa na serikali katika kuimarisha
nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa lengo la kuhakikisha wananchi
hasa wafuasi wa chama chetu wanaishi katika maisha mazuri na yenye
heshima yanayoendana na hadhi ya rasilimali tulizonazo”., alisema
Masauni na kusisitiza kuwa maendeleo hayana itikadi za vyama , kabila na
dini hivyo kila mtu anatakiwa kutoa ushirikiano kwa chama na serikali
katika mipango ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Masauni
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi aliwataka vijana
nchini kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani badala yake wakae
pamoja na kubuni fursa za maendeleo zitakazowaingizia kipato.
Alieleza
kwamba uchaguzi mkuu umekwisha na kilichobaki kwa sasa ni wananchi
kuacha itikadi za kisiasa na kushirikiana kwa pamoja kujenga maendeleo
ya nchi.
“Naomba
Wananchi tujenge utamaduni wa kufanya kazi za siasa wakati wa uchaguzi
na ukimaliza tu basi sote mawazo na fikra zetu tuzielekeze katika
harakati za ujenzi wa nchi yetu.,” alisisitiza Masauni.
Akizungumza
Katibu wa Wilaya ya Mjini Kichama, Fatma Shomari alisema kwamba hali ya
kisiasa ndani ya wilaya hiyo imeendelea kuimarika toka kumalizika kwa
Uchaguzi wa Marudio wa machi 20, mwaka huu.
Alieleza
kwamba viongozi mbali mbali wa Chama na serikali hasa Wabunge,
Wawakilishi na Madiwani wamekuwa wakiendelea kutekeleza Ilani ya
Uchaguzi wa CCM ya mwaka 2015/2020, kwa juhudi kubwa hali inayojenga
matumaini kwa wananchi.
Katibu
huyo alisema Chama kinaunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali
katika kuimarisha mji wa Zanzibar ili uwe wa kisasa na unaoendana na
hadhi ya nchi.
“Tunaomba
wananchi waelewe kwamba serikali haina nia mbaya katika kutengeneza mji
wetu lengo ni kuweka mji katika mazingira safi na yenye muonekano wa
kisasa.” Alisema Fatma.
Akitoa
taarifa fupi ya hali ya kisiasa ndani ya Wilaya ya Amani Kichama,
Abdallah Mwinyi alisema wilaya hiyo ina jumla ya wanachama 25,998
,wanawake 15,309 na wanaume 10,689.
Alisema
katika juhudi za kuimarisha chama tokea mwaka 2012 hadi 2015 jumla ya
wanachama 13,565 sawa na asilimia 52 wamelipa ada katika maeneo mbali
mbali ya wilaya hiyo.
Mwinyi
alieleza kwamba utekelezaji wa ilani ya CCM ndani ya wilaya hiyo
umeendelea kwa kasi kubwa ikiwemo uchimbaji wa visima vya maji safi na
salama pamoja na ukarabati wa barabara za ndani katika Majimbo ya
Chumbuni, Magomeni na Shauri Moyo kwa lengo la kuwarahisishia wananchi
huduma za kijamii.
Katika
ziara hiyo, Masauni alitembelea na kuzindua miradi mbali mbali ya
maendeleo katika Wilaya ya Mjini ametembelea ujenzi wa Tawi la Mwembe
Ladu na kuchangia kiasi cha shilingi 500,000 pamoja na mradi wa ujenzi
wa uzio na mnara wa tanki la maji katika shule ya msingi Makadara.
Maeneo
mengine ni uzinduzi wa mradi wa Maji safi na salama katika tawi la CCM
Sebleni Mwembeboso uliogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni nane
pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara za ndani katika maeneo ya Boznia
hadi Maktaba Kuu Zanzibar iliyopo Kikwajuni.
Kwa
upande wa Wilaya ya Amani, ametembelea ujenzi wa barabara ya Ziwatuwe
hadi Shauri Moyo pamoja na kuweka jiwe la msingi katika Tawi la CCM
Shauri Moyo “B” na kuchangia kiasi cha shilingi 400,000.
0 comments:
Post a Comment