Wapiganaji
wa kundi a waasi la Free Syrian Army (FSA), wakipambana dhidi ya kundi
la Islamic State katika mji wa Dabiq, Oktoba 15, 2016.
Waasi wa
Syria wanaoungwa mkono na Uturuki wameuteka Jumapili hii Oktoba 16 mji
wa Dabiq, mji ulio karibu na mpaka wa Uturuki, ambao mpaka sasa ulikua
moja ya ngome kuu ya kundi la Islamic State kaskazini mwa jimbo la
Aleppo.
Mwezi
Agosti 2014, waasi hao walijikuta mji wao ukianguka mikononi mwa kundi
la Islamic State. Jumapili hii, wakazi wa mji wa Dabiq wamesema
kufurahishwa na kutimuliwa kwa kundi la Islamic State katika mji wao.
Kwa sasa kwa kuwa wanajihadi wametimuliwa kabisa katika mji huo,
shughuli za kukagua na kutegua mabomu yaliyotegwa ardhini zinaendelea.
Shirika
la Haki za Binadamu nchini Syria, limebaini kwamba 'waasi waliudhibiti
mji wa Dabiq baada ya kuondoka kwa wapiganaji wa kundi la IS'. Moja ya
makundi ya waasi limeeleza kwamba mapigano yalikua makali. Waasi tisa
waliuawa wakati wa mapigano hayo. Makundi mengine ya waasi yamebaini
kwamba upinzani wa kundi la IS ulikuwa 'mdogo'.
Kulingana
na imani ya Waislam wenye msimamo mkali, vita vya mwisho kati ya jeshi
la Waislam na makafiri vitatokea katika mji huu na itakuwa mwanzo wa
Kiyama. Ushahidi muhimu wa mji huu kwa wanajihadi, kundi la Islamic
State lililipa gazeti lake kuu jina la mji huu. RFI
0 comments:
Post a Comment