Mfumuko nchini Nigeria huenda umeathiri kampuni ya Dangote Group inayomilikiwa na mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote.
Kampuni hiyo imeripotiwa kuwafuta kazi wafanyikazi 48 wakiwemo wataalam 36 wa kigeni na raia 12 wa Nigeria.
Ripoti zinasema kuwa hatua hiyo inatokana na gharama ya juu ya kufanya
biashara katika taifa hilo na kampuni hiyo imeshindwa kupata fedha za
kigeni kuwalipa wafanyikazi hao wa kigeni.
Lakini msemaji wa Dangote Group Tony Chiejina aliambia BBC kwamba ufutaji huo hauna uhusiano na mfumuko.
Kampuni hiyo inasema kuwa ilikuwa inaimarisha biashara zake na kwamba kazi zengine zimechukuliwa na kampuni tanzu.
Kampuni ya Dangote Group ni miongoni mwa kampuni zilizo na wafanyikazi wengi katika sekta hiyo.
Miezi miwili iliopita ,kitengo cha habari cha Bloomberg kiliripoti
kwamba bwana Dangote alipoteza dola bilioni 5.4 mwaka huu kutokana na
kuanguka kwa thamani ya sarafu ya Nigeria ,Naira.
Monday, October 24, 2016
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Mvua kubwa za El-Nino zilizonyesha zimeleta athari maeneo mbalimbali...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wakiwa wamejipanga tayari kwa maandamano katika maadhimisho ya S...
-
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment