Jokate
Mwegelo akiwasili katika shule ya Sekondari ya Majani Ya Chai ya
Vingunguti. Kulia kwake ni Mkuu wa shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi.
Jokate
Mwegelo akitoa hotuba yake katika Mahafali ya Nane ya Kidato cha Nne ya
Shule ya secondari ya Majani ya Chai. Katika Hotuba yake, Jokate alitoa
ahadi ya kuwajengea uwanja wa michezo na matundu ya Vyoo shuleni hapo.
Ujenzi huo utaanza baadaye.
Mkuu wa
Shule ya ya Sekondari ya Majani ya Chai, Kasango Pascal Ngozi akitoa
neno la shukrani baada ya ahadi ya Jokate Mwegelo wa kujenga uwanja wa
michezo na matundu ya vyoo.
Jokate
Mwegelo akimkimkabidhi zawadi ya kuwa mwanamichezo bora wa wanafunzi wa
kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Khalid Ibrahim
katika mahafali ya nane ya shule hiyo. Anayeshuhudia (wa kwanza) ni
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi.
Jokate
Mwegelo akimkimkabidhi zawadi mwanafunzi mwenye nidhamu bora kwa kidato
cha nne wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Khalid Ibrahim katika
mahafali ya nane ya shule hiyo. Anayeshuhudia (wa kwanza) ni Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi.
Jokate
Mwegelo akiserebuka na wanamuziki wa bongo fleva wanaosoma katika shule
ya sekondari ya Majani ya Chai wakati wa Mahafali ya Nane
yaliyofanyika juzi. Jokate ameahidi kuijengea shule hiyo uwanja wa
michezo na matundu ya vyoo.
Na Mwandishi wetu
Mrembo
mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake yake ya
kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” ameahidi kujenga
uwanja wa michezo kwa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai iliyopo
Vingunguti jijini.
Akizungumza
katika Mahafali ya Nane ya shule hiyo, Jokate alisema kuwa ameguswa na
changamoto mbalimbali zinazo ikabili shule hiyo na kuamua kusaidia kwa
kupitia kampeni yake hiyo.
Tayari Jokate amekabidhi viwanja vya netiboli na mpira wa kikapu kwa shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani.
Jokate
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, alisema kuwa serikali
peke yake haitaweza kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu
na nyinginezo na hivyo inahitaji msaada kutoka kwa sekta binafasi na
wadau.
“Nashukuru
kwa kunichagua kuwa mgeni rasmi katika mahafali haya, hii imenipa
faraja kubwa sana, nimesikia changamoto mbalimbali, kwa kuanzia nitaanza
kujenga uwanja wa michezo na matundu ya vyoo,” alisema Jokate.
Alisema
kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo
ya michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya
sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha
zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini.
Mkuu wa
Shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi alisema kuwa wanalazimika kutumia
viwanja vya shule jirani katika kufanikisha masuala ya michezo ambayo ni
moja ya masomo muhimu sana.
Ngozi
alisema kuwa wanatambua kuwa kuna vipaji kibao vya michezo katika shule
yao, lakini kutokana na kukosa viwanja bora wameshindwa kuvitambua.
“Tunashukuru
Jokate kwa ahadi ya kutujengea uwanja wa michezo na matundu ya vyoo,
hii itatoa hamasa kwa wanafunzi wenye vipaji katika michezo mbalimbali
kutambuliwa na vile vile kuendelezwa, bado tuna tatizo la jengo la
utawala, samani za ofisini na kumalizia uzio wa shule, tunawaomba wadau
watusaidie kufanikisha hayo,” alisema Kasango.
Mahafali hayo yalipambwa na burudani mbalimbali za muziki wa bongo fleva, singeli, ngoma kutoka kwa wanafunzi wa shule hiyo.
0 comments:
Post a Comment