Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme- TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kulia)
akiwaelekeza jambo watumishi wa TEMESA Arusha alipotembelea kituoni hapo
kutoka kushoto waliosimama ni Meneja wa TEMESA Arusha Mhandisi Heriel
Mteri, katikati ni Mhasibu wa TEMESA Arusha ndugu Simon Ringia na kulia
ni Mhasibu Msaidizi wa TEMESA Arusha Bi. Rebecca Temba.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kulia)
akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Karakana ya Magari chuo cha Ufundi Arusha,
Bw. Joseph Kotini wakati alipotembelea chuo hapo.
Mtendaji
Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu(kulia) pamoja na Mkuu wa Karakana ya
Magari chuo cha Ufundi Arusha Bw. Joseph Kotini wakiangalia shimo
linatumika kukagua na kufanya matengenezo madogo ya magari chuoni hapo.
Mkuu wa
Karakana ya Magari Chuo cha Ufundi Arusha Bw. Joseph Kotini (kushoto)
akitoa maelezo kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu juu ya
mtambo unaotumika kufanya ukaguzi na matengenezo makubwa ya magari
chuoni hapo. Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Arusha.
Na Theresia Mwami TEMESA Arusha
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu ameahidi
kuziimarisha karakana zilizopo chini ya TEMESA ili kuimarisha utendaji
kazi.
Mikakati
hiyo imetolewa leo na Mtendaji huyo alipokutana na watumishi TEMESA wa
mkoani Arusha alipotembela kituo hicho kuangalia utendaji kazi wa kituo
hicho.
“Naahidi
kushirikiana nanyi katika kuijenga TEMESA Mpya na naomba ushirikiano
wenu na muwe wafuatiliaji wa mambo kwani kazi zetu zinahitaji sana
ufuatiliaji wa kina” Alisema Dkt Mgwatu.
Ameongeza
kuwa amepanga mikakati namna ya kuyatambua madeni ya TEMESA pamoja na
utunzaji wa taarifa zake, kufanikisha utendaji kazi wa baadhi ya
karakana,kuwezesha urahisi wa mawasiliano kati ya TEMESA makao makuu na
vituo mikoani.
Amesisitiza
kuwa watumishi wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa dhana
potofu iliyojengwa juu ya TEMESA kwa wateja wake kuwa wanafanya kazi kwa
mazoea, wajiimarishe katika utendaji kazi kwa kasi, ubora, weledi
uadilifu, ufuatiliaji, na uwajibikaji.
Katika
hatua nyingine Dkt. Mgwatu ametembelea Chuo cha Ufundi Arusha ili
kujionea shughuli mbalimbali za mafunzo yanayotolewa chuoni hapo na
amefurahishwa na vifaa vya kisasa vya kutengenezea magari vinavyotumika
katika karakana ya chuo hicho kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa
wanafunzi wake.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Richard Masika alionesha nia ya
kushirikiana kwa ukaribu na TEMESA ili kuweza kuboresha mafunzo ili
kupata huduma zinazotolewa katika karakana za TEMESA.
0 comments:
Post a Comment