JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limehitimisha maadhimisho
ya miaka 52 ya kuasisiwa kwa jeshi hilo, kwa kuonesha zoezi la medani
liitwalo ‘Amphibious Landing’ lililofanyika Bagamoyo, Pwani.
Tukio hilo lililokuwa na mvuto wa aina yake, lilifanywa juzi jioni
katika kijiji cha Baatini huku likishuhudiwa na Rais John Magufuli, Rais
wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa, Dk Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi na
Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Abdulhamid Yahaya Mzee.Katika mazoezi hayo ya wiki mbili, Jeshi lilionesha uhalisia, jinsi wanavyoweza kukomboa eneo lililotekwa.
Wakati wa zoezi hilo, Meja Patrick Sawala alikuwa akielezea mtiririko wa
matukio kwa Rais Magufuli na baada ya vikosi kumaliza kazi ya kukomboa
eneo lililotekwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali, Davis Mwamunyange
alisema anajivunia kuwa kiongozi wa chombo hicho.
‘Najivunia kuwa kiongozi wa chombo hiki, kwa sababu nina askari na
maofisa wazuri, wanaojituma sana, weledi, wazalendo na wako tayari
kulinda watanzania na wanafanya hivyo kwa maslahi ya nchi yao, na hata
nje ya nchi tunajivunia kwa sifa yetu ya nidhamu na uimara wetu,”
alisema Mwamunyange.
Mwamunyange alimwambia Rais Magufuli kuwa vifaa hivyo vya kijeshi ni
mali ya watanzania, vimenunuliwa na watanzania na vyote vinaendeshwa na
watanzania wenye maadili na weledi na nidhamu ya hali ya juu kwa nchi
yao.
Katika mazoezi hayo, jeshi lilitumia ndegevita, vifaru vyenye uwezo wa
kukaa baharini na kutembea nchi kavu, melivita, boti za kasi.
Akizungumzia lengo la mafunzo na zoezi hilo lililoshirikisha kamandi ya
anga, maji, nchi kavu na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Mwamunyange
alisema ni kuimarisha ushirikiano na utendaji kazi wa vikosi. Rais
Magufuli ambaye alivalia mavazi ya kijeshi, hakuweza kuficha hisia zake
baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, alisema ameridhika na uwezo wa jeshi
hilo.
“Niseme ukweli, nimeridhika, hakuna anayeweza kutuchezea, tuna jeshi
imara sina mashaka niko salama na watanzania wako salama,”alisema Rais
Magufuli.
Mbali ya kulisifia jeshi kwa kazi nzuri inayofanya, pia aliahidi kutatua
changamoto mbalimbali zinazokabili chombo hicho na kusema fedha za
mafungu ya matumizi (OC) katika vyombo vyote vya ulinzi na usalama,
zitaongezwa.
Saturday, October 1, 2016
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akizungumza na watumishi wa Mkoa wa Rukwa (hawapo pichani) Wakuu wa taasisi mba...
-
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry Muro akipokea maelezo ya jinsi zoezi la sens...
-
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (Mb)akisisitiza umuhimu wa Taaisisi za Serikali ambazo hazijawsilisha gawio na michango yake...
-
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertili...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment