Staffan De Mistura amesema kuwa anatarajia usambazaji wa misaada kuanza hivi karibuni
Vikosi
maalum vya umoja wa mataifa nchini Syria vimesema vimeridhishwa na
kupungua kwa mapigano tangu usitishwaji wa mapigano kuanza siku ya
jumatatu.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Staffan De Mistura amesema kuwa anatarajia usambazaji wa misaada kuanza hivi karibuni,
Vikosi maalum huko Syria vimesema kuwa kuna utulivu maeneo mengi ya nchi
Amesema pia kipaumbele cha sasa ni kuandaa usambazaji wa misaada katika maeneo yaliyoshikiliwa na waasi huko Aleppo.
Mistura
ameonya kuwa usitishwaji wa mapigano unaweza kuhatarishwa na athari za
matukio ya vurugu yanayohusisha pande zenye mzozo.
Kwa mara ya kwanza imeripotiwa kutokuwepo kwa mauaji ya raia
Wizara ya mambo ya nje ya Syria imeonya kuwa vifaa havitaruhusiwa kuingia Aleppo bila ruhusa yake.
Kusitishwa
kwa mapigano kumeleta utulivu katika maeneo ya wakazi yanayoshikiliwa
na waasi mjini Aleppo huku watoto wakicheza nje kwa mara ya kwanza bila
kuwepo kwa ndege za mashambulizi, lakini Urusi imeshutumu waasi kwa
ukiukaji zaidi ya mara ishirini nchi nzima wa makubaliano ya kusitisha
mapigano na kuitaka Marekani kuweka nguvu kwa kundi wanalounga mkono.
Vikosi
maalum huko Syria vimesema kuwa kuna utulivu maeneo mengi ya nchi tangu
kuanza kwa usitishwaji wa mapigano wa muda siku ya jumatatu.
Mkuu wa
shirika la misaada la Islamic Relief huko Syria, Ahmed Mohamoud
ameiambia BBC kuwa kuwa shirika lake litafanya kila liwezakano lakini
ana mashaka juu ya usitishwaji wa mapigano kuendelea.
"Ukilinganisha
na siku zilizopita, hakuna shaka vurugu zimepungua. Ukizingatia ni
masaa 24, kwa masaa 48 ya usitishwaji yatakua muhimu sana kwasababu hiyo
ni tathmini kwa pande zote mbili kuhusu kiwango cha kupungua kwa
uhasama kwa jinsi walivyokubaliana siku ya ijumaa usiku" Staffan De
Mistura, Mjumbe wa umoja wa mataifa Syria
BBC
0 comments:
Post a Comment