Nchi hizo
zimeshindwa kufikia muafaka juu ya namna ya kufufua makubaliano ya
kusitisha mapigano Syria. Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, John
Kerry, sasa aelekea kukata tamaa kuhusu amani kurejea.
Hayo
yamejitokeza katika Syria mkutano ambao mwakilishi wa Umoja wa Mataifa
katika mzozo wa Syria Stefan de Mistura ameuita wenye machungu, mgumu na
wenye kukatisha tamaa.
Kundi la
kimataiafa linaloiunga mkono Syria, ikiwemo Marekani, Urusi na mataifa
mengine yenye nguvu, lililikutana kandoni mwa mkuno wa mwaka wa Umoja wa
Mataifa, unaowakutanisha viongozi wa ulimwengu mjini New York wakati
jeshi la Syria likiwa limetangaza kuanza mashambulizi mapya ya kijeshi
katika eneo linalodhibitiwa na waasi mjini Aleppo.
Kauli ya kukata tamaa ya Kerry
Waziri wa
Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amesema amesema amekatishwa tamaa,
na kwamba ari yake katika mazungumzo imepungua, ikilinganishwa na siku
iliyotangulia.
Lakini
mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov amesema upinzani nchini Syria unapaswa
kuchukua hatua katika kufikia makubaliano. Kerry anasema Marekani na
washirika wake ambao wanayaunga mkono makundi ya upinzani wako tayari
kurejea katika mazungumzo lakini pale tu Urusi itaonesha nia thabiti ya
kutekeleza makubaliano ya kuweka chini silaha.
Mashambulizi zaidi Aleppo
Ndege za
kivita zimefanya mashambulizi makali katika wilaya zinazodhibitiwa na
waasi nchini Syria na kufifisha matumani ya kumaliza vita vya wenyewe
kwa wenyewe vilivyoanza 2011. Maafisa kwa upande wa uasi wanasema mabomu
ni miongoni mwa silaha zilizovurumisha mjini Aleppo.
Hamza
al-Khatib, mkurugenzi wa hosiptali moja katika eneo ambalo linadhibitwa
na waasi upande wa mashariki wa mji huo anasema watu 45 wameuwawa.
Katika
hatua nyingine Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeipa timu ya
uchunguzi ya kimatiafa wiki tano zaidi kukamilisha ripoti yake
itakayoeleza nani anayestahili kubeba lawama kufuatia mashambulizi ya
gesi ya sumu nchini Syria kitendo ambacho Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ufaransa, Uingereza na mataifa mengine yanasisitiza adhabu kali
kwa wale waliohusika na kitendo hicho.
Timu hiyo
ilipaswa kuwasilisha ripoti yake juma hili, lakini Ban aliyaambia
mataifa 15 wanachama katika barua yake ambayo shirika la habari la
Reuters limeiona kwamba waandaaji wanahitaji muda wa ziada na kutaka
icheleweshwe hadi Oktoba 21. Baraza limeongeza muda huo mpaka Oktoba 31.
Ripoti ya
hivi karibuni kabisa ya baraza la usalama la umoja wa matiafa
iliyotolewa mwezi uliopita juu ya uchunguzi wa shirika la umoja huo
lenye kudhibiti silaha za kemikali OPCW inaeleza kuwa serikali ya Syria
ilihusika na mashambulizi mawili ya gesi ya sumu na Kundi la Dola la
Kiislamu lilitumia aina nyingine ya gesi ya sumu. DW
0 comments:
Post a Comment