Rais wa
chama cha UNC, Vital Kamerhe, akihojiwa na vyombo vya habari wakati wa
ufunguzi wa mazungumzo. Ni msimamizi msaidizi wa mazungumzo kutoka
upande wa upinzani unaoshiriki mazungumzo hayo.
Kiongozi
wa ujumbe wa upinzani Vital Kamerhe ndiye alitangaza uamuzi huo alipokua
akiondoka katika tume pana inayosimamia mazungumzo hayo. Tume ya
uchaguzi itajadili kalenda ya uchaguzi na daftari la uchaguzi, masuala
mawili muhimu katikal mazungumzo hayo.
Ujumbe wa
upinzani ulionya kwamba kuna mistari nyekundu haitakiwi kuvukwa, hasa
uchaguzi wa urais na wa wabunge unapaswa kupangwa katika nafasi ya
kwanza. Inafahamika kwamba chama tawala na vyama vinavyokiunga mkono
wana maoni tofauti na wanabaini kwamba uchaguzi wa serikali za mitaa
ndio unapaswa kufanyika, kwa hiyo itakua ni kurudi nyuma na kwamba sio
lazima kuachana na uchaguzi huu.
Wito kwa jumuiya ya kimataifa
Kwa
upande wake Vital Kamerhe, kiongozi wa chama cha UNC na kiongozi wa
ujumbe wa upinzani, anasema jukumu kwa kushindwa kuandaa uchaguzi ni
kutokana na serikali. Hata hivyo, azimio 22-77 limekua likitoa
kipaumbele kwa uchaguzi wa urais, na ule wa wabunge, na inatakiwa
jumuiya ya kimataifa kuheshimu maandiko ambayo ni muhimu katika
mazungumzo haya, yaani Katiba, azimio 22- 77 na Mkataba wa Umoja wa
Afrika.
Serikali
na vyama vinavyoiunga mkono wanasema tume ya usuluhishi inatakiwa ifanye
kazi yake vilivyo. Kila upande umekua ukitoa msimamo wake. Kambi hiyo
inajiuliza iwapo tume ya usuluhishi utachagua kutumia azimio 22-77 na
makubaliano ya wote. RFI
0 comments:
Post a Comment