MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi huku wananchi wakiwa kwa pembeni
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akifurahia jambo na viongozi wa wilaya ya mufindi
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa na viongozi wa wilaya ya mufindi wakiangalia muonekano wa wa gari hilo la kubebea wagonjwa
na hii ndio sehemu ya ndani ya gari la kubebea wagonjwa alilokabizi mbunge wa Mufindi kaskazini,Mahamood
Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi.
na fredy mgunda,iringa
Gari
la kubebea wagonjwa [Ambulance] lenye thamani ya mill.80 lakabidhiwa katika kwa
mkurugenzi na mkuu wa wilaya wa Mufindi na MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood
Mgimwa ametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya
matumizi ya hospitali ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo
lake hilo.
Mgimwa alikabidhi gari hilo
ikiwa ni moja ya ahadi yake aliyoitoa wakati akiomba kura kwa wananchi wa jimbo
la mufindi kaskazini katika kampeni ya uchaguzi mkuu 2015,ambapo alisema kutokana
na changamoto ya uhaba wa gari ya kubebea wagonjwa katika zahanati na vituo vya
afya katika jimbo hilo, endapo atapewa ya kuwa mbunge atahakikisaha
gari ya wagonjwa linapatikanaili wagonjwa waweze kufika hospital kwa wakati.
Akizungumza
na wananchi wakati wa kukabidhi gari hilo,mbunge Mgimwa alisema muda wa
kupiga siasa umeshapita na kazi iliyopo hivi sasa ni kuwaletea wananchi
maendeleo kwa kuwatatulia changamoto zinazowakabili.
Alisema
pamoja na kuongeza gari ya wagonjwa atahakikisha anaboresha vituo vya
Afya vilivyopo katika jimbo lake ili kupunguza wimbi kubwa la msongamano
wa wagonjwa wanaokuja kutibiwa katika Hospitalini ya wilaya.
‘’’Nipo
kwenye mchakato wa kuboresha vituo vyote vya Afya ndani ya jimbo langu,na
nitahakikisha huduma muhimu zinapatikanaikiwa pamoja na dawa za kutosha na
vifaa mbalimbali vinavyohitajika ili wananchi wangu waweze kuhudumiwa bila
usumbufu katika vituo hivyo,hii itasaidia kupunguza msongamano katika hospitali
ya wilaya’’’’’alisema Mgimwa
Aidha
katika mkutano huo mbunge alisisitiza swala la uaminifu kwa watumishi waliopewa
dhamana ya kuwatumikia wananchi wahakikishe wanajikinga na vitendo
vinavyoashiria rushwa ,vinavyoweza kuwaharibia sifa ya utendaji kazi zao na
kushindwa kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao.
‘’’Sisi
wabunge,madiwani na mtumishi yeyote aliyepewa dhamana na wananchi anatakiwa
ajiepushe na swala zima la rushwa ili aweze kutenda haki kwa kuwatatulia
changamoto wananchi wake
waliomchagua. Tunatakiwa tuwatumie
wananchi kuwaletea maendeleo ipasavyo na si vinginevyo’’’alisema
Jamhuri
William ni mkuu wa wilaya ya Mufindi,akipokea msaada wa gari hilo kutoka kwa
mbunge Mgimwa alisema gari hilo litaweza kusaidia kuokoa vifo vya
wanamufindi hasa mama na mtoto ambapo
hapo awali kuliwa na gari moja tu.
Williamu
alisema kutokana na uwingi wa wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika hospitali ya
wilaya kwa mwezi ni zaidi ya 500 aliosimia kubwa ni akina mama wajawazito na
wengi wao wanafikishwa wakiwa katika hali
mbaya kutokana na gari la wagonjwa kuwa moja na kushindwa
kumudu.
“Tunamshukuru
mbunge kwa kuliona hili na na kuokoa maisha ya watu hasa mama na mtoto ingawa
bado hitaji lipo kutokana na uwingi wa wagonjwa endapo tutapata gari
la tatu itasaidia sana”alisema
Williamu
ameongeza kwa sasa gari hilo litahudumiwa na wilaya kuanzia kuwalipa
wafanyakazi wa gari hilo,kulifanyia marekebisho ya gari hilo endapo litatokea
kuharibika kwa aina yoyote ile.
Wananchi
nao walitoa malalamiko yao kwa mbunge Mgimwa,ambapo Markusi Chusi alimuomba
mbunge aweze kusiomamia swala la utapikananji wa vibali vya kuvuna miti,kwa
kumtaka ahakikishe wazawa wa eneo husika wanapewa kipaumbele ili waweze
kunufaika mali alisi hiyo ilipo kwako.
‘’’’Tumelia
kwa muda mrefu,sisi tunanyanyasika kwa kuwapendelea wageni na kutuacha sisi
wenyeji tuliopo hapa.Nimeomba mara tano hivi sasa na ukizingatia mimi ni mjane
lakini naachwa na pesa yangu inaliwa wageni wanapewa hali
inayotukatisha tama wananchi tuliouzunguka msitu huu.’’’’alisema
0 comments:
Post a Comment