METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, September 23, 2016

TUMEDHAMIRIA KUWASAJILI WATOTO WOTE NCHINI – WAZIRI MWAKYEMBE

mwake
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akikata utepe kuzindua mpango huo kwa ajili ya mikoa ya Iringa na Njombe katika viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwasajili watoto wote nchini wenye umri chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa.
Dhamira hiyo ya Serikali inalengo la kuiondoa nchi katika takwimu zinazoonyesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwisho barani Afrika ambazo watoto hawana vyeti vya kuzaliwa.

Dkt Mwakyembe amesema hayo mjini iringa alipokuwa akizindua kampeni ya uandikishaji watoto chini ya miaka mitano katika mikoa ya Iringa na Mbeya iliyofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa.

Dkt Mwakyembe ameelezea kusikitishwa na kitendo hicho cha kuwa miongoni mwa nchi ambazo watoto wake hawajasajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa na kusema kuwa ndio maana kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikaamua kuendesha kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano.

Amesema serikali imedhamiria kuiondoa Tanzania katika hali hiyo kwakuwa sio sahihi kwa nchi kuwa katika nafasi hiyo sawa na Somalia

‘Hali hii sio sahihi, Tanzania haistahili kuwepo katika kundi hilo tumedhamiria kuiondoa nchi huko, tunataka Tanzania iwe juu ktk usajili wa watoto kama ilivyo juu kwa chanjo mbalimbali kwa watoto wetu’ alisema.

Mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuhakikisha watoto wote chini ya miaka mitano wanasajiliwa na kuwa ma vyeti vya kuzaliwa unaendeshwa kupitia Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi RITA chini ya ufadhili wa UNICEF.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com