Washukiwa wa ugaidi waliokamatwa nchini Uganda
Jaji wa
Mahakama maalum inayoshughulikia kesi za uhalifu wa Kimataifa katika
Mahakama kuu jijini Kampala nchini Uganda, ametishia kuwaachilia huru
washukiwa wa ugaidi kutoka kundi la Al Shabab nchini Somalia.
Jaji
Elizabeth Nyahamya amesema washukiwa hao nane wataachiliwa huru ikiwa
serikali itashindwa kuanza kesi dhidi yao kama ilivyoahidi.
Washukiwa
hao wamekuwa wakifika Mahakamani mara kwa mara lakini hawafunguliwi
mashtaka, hali ambayo imewakera mawakili na washukiwa wenyewe.
Kiongozi
wa mashtaka Rachael Bikoli anayeiwakilisha serikali katika kesi hii,
ameiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe 15 mwezi Desemba
atakapokuwa tayari kuwafungulia mashitaka washukiwa hao.
“Umesema
kwa mdomo wako mwenyewe kuwa, kesi hii itaanza tarehe 15 mwezi Desemba,
sitaahirisha tena kesi hii, ikiwa haitaanza, sitakuwa na lingine bali
kuwaachilia huru washukiwa hawa kwa sababu hakuna ushahidi,” alisema
Jaji Nyahamya.
Washukiwa
hao raia wa Somalia wametajwa kuwa; Mohamed Abdulkadir Hirsi
anayejulikana kwa jina maarufuku kama Mohamed Abdul Aziz Adan, Abdi
Abdullahi Bootan, Hassan Abduwali Mohamoud, Mohamed Ahmed Gele, Yusuf
Osman Hussein, Abdi Ali, Abdul Kadir Mohamed Mohamud Sandir na Mohamad
Yusuf Farah.
Washukiwa hao walikamatwa mwaka 2014 na wamekuwa wakizuiliwa bila ya kufunguliwa mashtaka ya ugaidi kwa muda huo wote.
RFI
0 comments:
Post a Comment