METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, September 16, 2016

Hillary Clinton arejea kwenye mbio za kampeni

Clinton aliishiwa nguvu wakati wa kumbukumbu ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11
Clinton aliishiwa nguvu wakati wa kumbukumbu ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11
Mgombea Urais kupitia Chama cha Democratic nchini Marekani Bi Hillary Clinton amerejea kwenye mbio za kampeni baada ya kuugua homa ya mapafu.
Akiongea na mwandishi wa habari akiwa kwenye ndege kuelekea Greensboro North Carolina, Bi Clinton alisema anajiskia vizuri baada ya mapumziko ya siku tatu.
Mpinzani wake wa Chama cha Republican, Donald Trump ametoa barua kutoka kwa daktari wake ikionesha kuwa ana afya njema.
Barua hiyo inaonesha kuwa anatumia dawa ili kupunguza unene na kiwango kilichopitiliza cha uzito, lakini hatumii kilevi wala kuvuta sigara.
Trump aliwahi kuwa mchekeshaji wa vipindi vya runinga
Trump aliwahi kuwa mchekeshaji wa vipindi vya runinga
Uchaguzi wa Marekani utafanyika mwezi Novemba ambapo kampeni zake zimekuwa na vuta ni kuvute kutoka vyama vikubwa viwili vya Democratic na Republican. BBC
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com