Bi Clinton akisaidiwa kuingia katika gari
Mgombea
Urais kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton amekutwa na ugonjwa wa
homa ya mapafu baada ya kuugua katika tukio la kuwakumbuka wahanga wa
shambulio la septemba 11.
Daktari wake Lisa Bardack amesema kuwa bi Clinton amekutwa na ugonjwa huo tokea Ijumaa.
Akijerea baada ya kupata nafuu
Amesema
pia Clinton aliongezeka joto na kuishiwa na maji mwilini katika tukio
hilo la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.
Clinton
aliondoka mapema, picha zilizowekwa mtandaoni zinamuonesha akisaidiwa na
msaidizi wake, huku akitaka kuanguka alipokaribia kwenye gari, lakini
baadae bi clinton alitokea kwenye nyumba ya mwanae na kuwaambia
waandishi wa habari kuwa anajisikia vizuri.
Donald Trump alihudhuria hafla hiyo
Awali mgombea Urais kupitia chama cha Republican Donald Trump alionesha wasiwasi juu ya afya ya hasimu wake.
Katika shughuli hiyo majina karibu elfu tatu ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11 yalisomwa. BBC
0 comments:
Post a Comment