TAARIFA
Jumuiya ya Wazanzibari Nchini Marekani (ZADIA), imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.
Mzee
Jumbe aliyewahi kuwa rais wa Zanzibar na Makamo wa Kwanza wa Rais wa
Tanzania, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika harakati za kuleta
maendeleo na mabadiliko ya kisiasa visiwani Zanzibar.
Chini
ya Uongozi wake, kwa mara ya kwanza Zanzibar ilipata katiba yake na
hivyo kuanzishwa kwa Baraza la Wawakilishi kama chombo cha uwakilishi wa
Umma na kutunga sheria.
Atakumbukwa
pia kwa msimamo wake shupavu wa kupigania haki sawa ndani ya Mungano wa
Tanganyika na Zanzibar khususan madai yake ya kutaka kuwa na serikali
tatu.
Marehemu
Jumbe alikuwa rais wa Zanzibar kuanzia mwaka 1972 kufuatia kifo cha
rais wa kwanza wa Zanzinbar Marehemu Abeid Aman Karume. Alilzaimishwa
kujiuzulu nyadhifa zake zote za kisiasa mwaka 1984 baada ya kutuhumiwa
kuchafua hali ya hewa ya kisisasa Zanzibar. Uchafuzi ambao si chochote
ila ushupavu wake wa kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya Muungano wa
Tanzania.
Kwa mnasaba huu, ZADIA inatoa mkono wa pole kwa Wazanzibari wote kwa ujumla kwa kuondokewa na kiongozi wao mzalendo.
Aidha
kono wa pole makhasusi uwafikie wanafamilia ya Marehemu, tukimwomba
Mwenyezi Mungu Mtukufu awape subira katika kipindi hiki kigumu cha
msiba, na kumwomba Mola Mlezi amlaze marehemu mahali pema Peponi. Amin.
Omar H Ali, Mwenyekiti, ZADIA
Agosti 14, 2016
0 comments:
Post a Comment