Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(katikati), akizungumza na
watendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za
Kulevya na Uhalifu(UNODC), Bi. Kaitlin Meredi (kulia) na Johan
Kruger(kushoto), walipomtembelea ofisini kwake,jijini Dar es
Salaam,jana. Ziara hiyo ikiwa na lengo la kujadili njia muafaka za
kukabiliana na biashara, matumizi na athari za dawa za kulevya kwa
jamii.
Mkuu wa
Kitengo cha Kupambana na Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya kutoka
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na
Uhalifu(UNODC),Johan Kruger(kushoto), akizungumza na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati),walipomtembelea ofisini kwake
kwa ajili ya kuzungumzia juhudi mbalimbali za kupambana na biashara
haramu ya Dawa za Kulevya.Kulia ni Mratibu wa Kupambana na Uhalifu wa
Majini, Kaitlin Meredith.
Mratibu
wa Programu ya Kupambana na Uhalifu wa Majini kutoka Shirika la Umoja
wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Kaitlin
Meredith (kulia), akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba, masuala yanayohusu udhibiti wa uhalifu unaofanyika
majini walipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, jana.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati),akiagana na Mratibu wa Programu ya Kupambana na Uhalifu wa Majini, Kaitlin Meredith, mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa waziri, jijini Dar es Salaam, jana.Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Johan Kruger (Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
0 comments:
Post a Comment