Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiteremka kuelekea eneo la
kuchinjia ng’ombe katika kiwanda cha nyama Ngulu Hills Ranch kilichopo
Morogoro wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakikagua eneo la kuchinjia
ng’ombe katika kiwanda cha nyama cha Nguru Hills Ranch cha Morogoro
Agosti 3, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi na Mshauri wa Kiwanda hicho,
Danstan Mrutu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizingumza na Mkurugenzi na
mshauri wa kiwanda cha nyama cha Ngulu Hills Ranch cha Morogoro ,
Dunstan Mrutu (kulia kwa Waziri mkuu) ) wakati walipokitembelea kiwanda
hicho Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Watoto na
wananchi wa kijiji cha Majichumvi wilayani Mvomero wakionyesha mabango
wakati WaziriMkuu,Kassim Majaliwa aliposimama kijijini kwao
kuwasikiliza Agosti 3, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni wa LAPF, Eliud Sanga wakati
alipokagua ujenzi wa stendi mpya ya Msamvu Morogoro Agosti 3, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua jengo la Stendi mpya ya mabasi la Msamvu
mjini Morogoro Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mjini Morogoro baada
ya kukagua ujenzi wa stendi mpya ya Msamvu Agosti 3, 2016. Kulia ni Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Dkt.Stephene Kebwe na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF,Eliud Sanga. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Awamu ya
kwanza ya jengo la stendi mpya ya mabasi ya Msamvu mjini Morogoro
iliyokamilika kwa asilimia 90. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliitembelea
stendi hiyo na kuzungumza na wadau Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Halima Mwishehe alipouliza swali
wakati Waziri Mkuu alipozungumza na Wananchi kwenye stendi mpya ya
Msamvu Morogoro baada ya kukagua ujenzi wake Agosti 3, 2016. Kulia ni
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka wafugaji wenye mifugo mingi nchini
kujiweka tayari kwa ajili ya kuhamia kwenye maeneo yatakayotengwa na
Serikali katika ranchi mbalimbali nchini ili waweze kufuga kisasa.
Pia
aliwataka wafugaji hao kushirikiana na Serikali katika kuboresha
miundombinu ya maeneo hayo ikiwemo ujenzi wa visima vya maji na majosho
ili ufugaji wao uwe na tija.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati
alipotembelea kiwanda cha kusindika nyama cha Nguru Hills Ranch
kilichoko wilayani Movomero.
Hata
hivyo Waziri Mkuu alisema kitendo cha wafugaji hao kuhamia katika ranchi
kitawezesha mifugo yao kuwa na ubora kwa sababu aina ya ufugaji wa sasa
ya kutembeza mifugo umbali mrefu inasababisha ufugaji wao kuwa na tija
ndogo.
Akizungumzia
kuhusu uwepo wa kiwanda cha kuchakata nyama wilayani Mvomero Waziri
Mkuu alisema kitamaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima na
wafugaji kwa kuwa wafugaji watapata fursa ya kuuza mifugo yao kiwandani
hapo.
“Uwepo wa
viwanda katika maeneo yetu utatuwezesha kupunguza matatizo tuliyonayo
katika maeneo yetu ikiwemo suala la migogoro kati ya wafugaji na
wakulima. Viwanda ndiyo vitakavyotuondoa kutoka katika uchumi wa chini
hadi wa kati,” alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi na Mshauri wa kiwanda cha Nguru Hills Ranch,
Dunstan Mrutu alisema kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe
300, mbuzi na kondoo 1,500 kwa siku kinatarajiwa kufunguliwa mwezi
Desemba mwaka huu.
Mkurugenzi
huyo alisema takriban asilimia 80 ya nyama itafungashwa na kuuzwa nje
ya nchi hasa Uarabuni kwa sababu nyama ya mbuzi ya Tanzania imebainika
kuwa na mvuto maalum katika nchi hizo.
“Mbali na
uwekezaji huu wa kiwanda cha nyama pia tunatazamia kuwekeza katika
mnyororo wa thamani kuanzia kusindika ngozi inayotoka kiwandani hadi
kuzalisha viatu, mikanda na bidhaa zote za ngozi na kupunguza uagizaji
wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi,” alisema.
Mrutu
alisema nia yao ni kuitikia wito wa Rais Dk. John Magufuli wa kutaka
viwanda vizalishe viatu nchini kuanzia vya majeshi na wananchi wote
ambapo wamepanga kuanzia mwakani wataanza kuuza bidhaa hizo.
Aliongeza
kuwa uwepo wa kiwanda hicho utatoa fursa kwa wafugaji na wakulima kuuza
majani, mifugo na mazao ya chakula kama mtama, mahindi, ambapo tayari
wameanza kuhamasisha jamii za wafugaji na wakulima wa Mvomero,
Ngerengere na sehemu zinazozunguka eneo la kiwanda kuchangamkia fursa
hiyo.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mvomero
kufanya mapitio ya mashamba ili kujua wamiliki wake na kama
hawajayaendeleza wachukue uamuzi wa haraka wa kuyatwaa na kuyarudisha
mikononi mwa Serikali.
0 comments:
Post a Comment