Mapigano yameendelea Mosul kabla ya operesheni dhidi ya wanamgambo wa IS
Vikosi
vya Kikurdi nchini Iraq vimesema vimedhibiti Vijiji kadhaa karibu na mji
wa Mosul kutoka kwenye himaya ya wanamgambo wa Isalamic State, mji mkuu
ambao unashikiliwa na wanamgambo nchini humo.
Mapambano
yalianza alfajiri siku ya Jumapili, vikosi vikisaidiwa na mshambulizi
ya anga ya muungano wa majeshi yanayoongozwa na Marekani katika
operesheni ya kupambana na IS.
Vikosi vya serikali ya Kikurdi na Iraq vimekuwa vikiuzingira mji wa Mosul kabla ya mapambano ya kuutwaa mji wenyewe.
Mosul, mji wa pili kwa ukubwa nchini Iraq umekuwa ukidhibitiwa na Islamic State tangu mwezi Juni mwaka 2014.
Kamanda wa majeshi ya kikurdi amesema wanajeshi zaidi ya 5,000 wako kwenye Operesheni.Mapigano bado yanaendelea.
BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment