Katibu wa
Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam na kiongozi wa Kanisa la
Anglikana, Mchungaji,John Solom(aliyeshika kipaza Sauti) akisali
kuombea uwanja wa ndege wa Terminal III unaoendelea kujengwa jana jijini
Dar es Salaam uliopo katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Mradi wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TAA), Mhandisi, Mohamed Milanga
akitoa maelekezo kwa viongozi mbalimbali wa dini jijini Dar es Salaam
jana walipotembelea na kuombea uwanja mpya wa ndege unaoendelea kujengwa
wa Teminal III uliopo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere.
Sheikh wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum akiomba dua kuombea
uwanja wa ndege wa Terminal III unaoendelea kujengwa jana jijini Dar es
Salaam uliopo katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam. Wengine ni Viongozi mbalimbali wa Dini.
Katibu
Mkuu wa Kampuni wa Mamlaka ya Anga Tanzania, Jaji Ramdhan Maleta(Mwenye
tai Nyekundu) akitoa neno la Shukrani mara baada ya kumaliza ziara ya
viongozi mbalimbali wa dini waliotembelea katika uwanja wa ndege
unaoendelea kugengwa wa Terminal III jijini Dar es Salaam jana.
Picha na Yasir Adam, Globu ya Jamii.
0 comments:
Post a Comment