METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, August 16, 2016

Mwenyekiti wa NEC amtembelea Spika Wa Bunge JoB Ndungai amjulia hali


 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva  (kushoto) akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akimkabidhi  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.Picha na Benjamin Sawe-Maelezo

By Christina Njovu

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva leo amemtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai nyumbani kwake  Jijini Dar es Salam na kumjulia hali baada ya kurejea kutoka nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu.

Akiwa nyumbanikwaspika Jaji Lubuva pia amemkabishiMh. Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwaniya Mwaka 2015 na kumueleza kuwa kukamilika kwa ripoti hiyo ndio hitimisho la Uchaguzi Mkuu na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao. 

Kwa upande wake Mheshimiwa Ndugai ameipongeza hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya kuweka mikakati ya kushiriki katika maonyesho mbalimbali yakiwemo yale ya biashara SabaSaba na Nanenane katika kutoa elimu kwa wananchi.

Jaji Mstaafu Lubuva alikwenda kumjulia hali Ndugai ambaye kipindi  cha Bunge la Bajeti lililomalizika hivi karibuni, alikuwa nchini India kwa matibabu  na hivi sasa afya yake imezidi kuimarika.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com