Abubakar Shekau
Kiongozi
anayepigwa vita wa kundi la Boko Haram amesema kuwa bado ndiye
anayeliongoza kundi hilo licha ya taarifa ya kundi la Islamic State
kwamba ameng'olewa mamlakani.
Abubakar Shekau alipuuzilia mbali uamuzi wa IS kwamba Abu Musab al-Barnawi ndiye kiongozi mpya wa kundi hilo.
Shekau amemshtumu al_Barnawi kwa kujaribu kufanya mapinduzi dhidi yake.
Kundi la
Boko Haram linapigania kuipindua serikali ya Nigeria ili kutangaza
serikali ya Kiislamu katika eneo la kaskazini mwa taifa hilo.
Katika
kipindi cha miezi 18 iliopita,kundi hilo limepoteza eneo kubwa
lililokuwa likidhibiti baada ya kukabiliwa vilivyo na jeshi la Nigeria
na majirani zake.BBC
0 comments:
Post a Comment