MKAZI wa Kiwalani, Dar es Salaam Habiba Kassim(55) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashishitakiwa taka ya mauaji ya mume wake kinyume cha sheria.
Habiba, ambaye ni mkulima amesomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, John Msafiri kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali, Neema Moshi.
Moshi alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo, Julai 16 mwaka huu saa nne usiku maeneo ya Kiwalani Bombom Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam ambapo alimuua mumuwe aitwaye, Chamas Ibrahim kinyume cha sheria.
0 comments:
Post a Comment