Mkuu wa
wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akizungumza na waandishi kukemea hatua
ya kuahirishwa Baraza la Madiwani leo kwasababu za kutotimia akidi.
Mkuu wa
wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro amekemea kitendo cha kuahirishwa kikao
cha Baraza la Madiwani katika jiji la Arusha kuwa kinawanyima wananchi
haki ya kuwakilishwa katika baraza hilo linalojadili maendeleo.
Kikao
hicho kimeshindwa kufanyika baada ya madiwani 14 pekee kuhudhuria katika
ya madiwani 36 ambao ni wajumbe halali wa kikao hicho.Meya wa Jiji
hilo,Kalist Lazaro amesema amelazimika kuahirisha kikao hicho baada ya
akidi kushindwa kutimia huku akidai baadhi ya madiwani wamejificha
wakiogopa kukamatwa na polisi kwa kuhamasisha maandamano ya Septemba
Mosi.
Mkuu wa
wilaya amepinga kauli hiyo ya Meya na kusema akiwa Mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama amewasiliana na Mkuu wa polisi wa wilaya(OCD)ambaye
alikanusha taarifa za kutafutwa madiwani hao.
0 comments:
Post a Comment