METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, March 1, 2016

Wenger: Tusahau Man U tugange ya Swansea

31A6CE4D00000578-0-image-a-2_1456793960879
Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anasema kuwa kipigo cha 3-2 uwanjani Old Trafford hakifai kuwadumaza kwani nia na azimio lao ni kukata kiu cha kombe la ligi kuu ya Uingereza.
Arsenal wamebakia katika nafasi ya 3 lakini sasa wana alama 5 nyuma ya vinara wa msimu huu Leicester.


Tottenham walifanikiwa kupata ushindi dhidi ya Swansea 2-1 na kusalia katika nafasi ya pili wakiwa na alama 54 tatu zaidi ya The Gunners.

”Kwa hakika hatuwezi kujihurumia eti kwa sababu tuliambulia kichapo Old Trafford ,lazima tujifurukute na kuthibitishia wapinzani wetu kuwa tupo kwenye kinyang’anyiro cha kombe la ligi msimu huu.” alisema Wenger.

Arsenal wanaialika Swansea ambayo ipo nafasi ya 16 katika jedwali la ligi ya premia ya Uingereza uwanjani Emirate.

Huku zikiwa zimesalia mechi 9 pekee msimu huu ukamilike kila mechi na alama inaumuhimu mkubwa katika vilabu husika.

Wenger alisema ” Kimsingi kichapo hicho kina maana zaidi ya moja kwetu,,,matokeo kamili yatabainika mwisho wa msimu.

Wenger hata hivyo alikataa katakata kukubali kuwa walishindwa na kikosi cha chipukizi cha United.
”tangu lini De Gea amekuwa mchezaji chipukizi, hawa wachezaji waliigharimu United mamilioni ya pauni, Watizame Memphis Depay, Morgan Schneiderlin na Juan Mata hicho ni kikosi dhabiti.”alinuna Wenger

Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com