WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amewataka wananchi wa
visiwani Zanzibar kujitokeza kwa wingi Machi 20, 2016 ili waweze kupiga
kura kwa amani na utulivu bila kubughudhiwa na mtu yeyote.
Kitwanga
amesema kuwa ulinzi umeimarishwa na kuwataka wananchi visiwani humo
kujitokeza kwa wingi kuja kumchagua kiongozi wanaompenda siku ya
uchaguzi huo na watarejea nyumbani kwao salama mara baada ya kumaliza
kupiga kura.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na baadaye
kuzungumza na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Waziri Kitwanga
alisisitiza kuwa, vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa vizuri na
wananchi waondoe shaka kwani hawatakubali vurugu ya aina yoyote itokee.
“Jitokezeni
kupiga kura siku ya uchaguzi kwani ni haki yenu, nawahakikishia usalama
upo na wa hali ya juu, asijitokeze mtu yeyote akawatisha kutokuja
kupiga kura, tumejipanga vizuri na lengo letu kubwa kabisa ni kuwalinda
wananchi,” alisema Kitwanga.
Hata
hivyo Waziri Kitwanga alisema hakuna mwananchi yeyote anayehama
kwakuogopa vurugu siku ya uchaguzi bali watu wanasafiri kwasababu
mbalimbali ikiwemo hiki ni kipindi cha maandalizi ya Sikukuu ya Pasaka.
“Hali ya Pemba ni shwari na pia nataka kusisitiza nikiwa Waziri wa Mambo ya Ndani sijapata taarifa yoyote rasmi kama kuna watu wanakimbilia nchi jirani. Lakini hata hilo la watu kukimbilia msituni inabidi tujiulize Pemba kuna msitu mkubwa wa watu kwenda kujificha? Haya mambo ni ya kuzusha, watu waende wakajionee wenyewe,” alisema Kitwanga.
“Hali ya Pemba ni shwari na pia nataka kusisitiza nikiwa Waziri wa Mambo ya Ndani sijapata taarifa yoyote rasmi kama kuna watu wanakimbilia nchi jirani. Lakini hata hilo la watu kukimbilia msituni inabidi tujiulize Pemba kuna msitu mkubwa wa watu kwenda kujificha? Haya mambo ni ya kuzusha, watu waende wakajionee wenyewe,” alisema Kitwanga.
Alisema hakuna dalili yoyote ya watu wanaokimbia kutoka Zanzibar kukimbilia
Tanzania Bara kutokana na idadi ya wasafiri kati ya Bara na Zanzibar
kuwa ya kawaida.
Alisema kama kuna ongezeko lolote basi ni kutokana na
sherehe za Pasaka kukaribia na si suala la kuogopa uchaguzi kama
inavyoelezwa.
Waziri Kitwanga alisema yupo hapa Zanzibar ili
kuhakikisha maandalizi yote ya uchaguzi wa marudio Jumapili unafanyika
kama ulivyopangwa.
“Vitisho vinavyoendelea tulivitegemea, tunajua kama
kuna watu hawataki uchaguzi na wanatumia mbinu mbalimbali ikiwamo ya
milipuko kutisha watu. Wito wangu kwa watu wanaotaka kupiga kura
wajitokeze kwa wingi na usalama wao upo,” alisema waziri huyo.
0 comments:
Post a Comment