Wapiga kura wa Bunda Mjini
waliowasilisha maombi ya kuruhusiwa kukata rufaa nje ya muda, kupinga
matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Ester Bulaya dhidi ya Steven
Wasira, wamekumbana na kigingi kingine cha pingamizi.
Maombi
hayo namba 25 ya mwaka 2016 yaliwasilishwa na wapiga kura Magambo Masato
na wenzake watatu, wakiiomba mahakama hiyo iwaruhusu kukata rufaa nje
ya muda baada ya kutupiliwa mbali na mahakama kuu.
Pingamizi
hilo liliwasilishwa jana na wakili wa wajibu maombi wa pili na wa tatu,
Paschal Malulu akiiomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo kwa kuwa
kiapo kilichoambatanishwa ni batili kwa kuwa aliyeapa ni tofauti na
aliyethibitisha.
“Haya makosa yaliyofanyika ni makubwa mno,
kiasi cha kutokurekebishika, kwa sababu kiapo kimethibitishwa na wakili
Constatine Mutalemwa huku aliyeapa ni wakili James Kahangwa,” alidai
Malulu.
Alidai kiapo hicho kimekosa nguvu kisheria kwa mujibu wa
sheria Na. 19 (1) (2), ni lazima kiwe na mambo ambayo mtu anaweza
kuyathibitisha au kuyasimamia, hivyo hii sheria imekiukwa, kwa lugha
nyingine kiapo kimekosa uthibitisho.
Malulu alidai kuwa kuna sheria inayosimamia kiapo wala siyo Katiba kwa ujumla wake, kama alivyoitaja Mutalemwa.
Jaji
anayesikiliza shauri hilo, Rose Ebrahim aliahirisha shauri hilo hadi
Machi 14, mwaka huu atakapolitolea maamuzi pingamizi hilo.
0 comments:
Post a Comment