Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amewaagiza watumishi wasio na sifa za kuajiriwa kujiondoa kabla ya March 31 mwaka huu.
Kijuu
alitoa kauli hiyo jana wakati wa Makabidhiano ya ofisi baina
yake na mkuu wa mkoa wa zamani,John Mongella ambapo alisema
kwamba Tanzania inawatumishi hewa zaidi ya 2000, hivyo ana imani
hata Kagera wapo.
"Hao
watumishi hewa endapo watang'ang'ania kubaki katika vitengo
walivyopo nitawashughulikia wahusika wakuu wa vitengo hivyo," alisema
Aidha,
aliagiza wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kusimamia uundwaji wa
mabaraza ya usuluhishi kuanzia ngazi za kata hadi mkoa ili
kusimamia haki za wananchi.
Pia
aliwataka watumishi wa serikali mkoani humo kufahamu maudhui ya
"Hapa Kazi Tu", kwa kufanya kazi kwa kasi,haraka, nguvu, maarifa na
uadilifu.
Aliwataka
kutosubiri kusukumwa, lakini wajitambue wao ni akina nani na
wanapaswa kufanya nini kutokana na majukumu waliyopewa.
Alisema
ili kufikia lengo la Rais John Magufuli la kuwatumikia wananchi
kwa uaminifu ni lazima kushikiria uadilifu na kutambua kwamba
watumishi wapo kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii.
0 comments:
Post a Comment